Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1884

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1884 ulikuwa wa 25 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 4 Novemba. Upande wa "Democratic Party", Grover Cleveland (pamoja na kaimu wake Thomas Hendricks) alimshinda mgombea wa "Republican Party" James Blaine (pamoja na kaimu wake John Logan).

Matokeo

hariri

Cleveland akapata kura 219 na Blaine 182. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.