Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1900

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1900 ulikuwa wa 29 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 6 Novemba. Upande wa "Republican Party", Rais William McKinley (pamoja na kaimu wake Theodore Roosevelt) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" William Jennings Bryan (pamoja na kaimu wake Adlai Stevenson).

Matokeo hariri

McKinley akapata kura 292, na Bryan 155. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.