Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1928

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1928 ulikuwa wa 36 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 6 Novemba. Upande wa "Republican Party", Herbert Hoover (pamoja na kaimu wake Charles Curtis) alimshinda mgombea wa "Democratic Party" Al Smith (pamoja na kaimu wake Joseph T. Robinson).

Matokeo

hariri

Hoover akapata kura 444, na Smith 87. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.