Uendelevu
Uendelevu ni hali ya watu kuishi vizuri na kwa usalama pamoja. Uendelevu unakuwa na maisha ya kila mtu na kila kitu. Uendelevu unakuwa na ujenzi, maduka, vyakula, maji, wanyama, misitu, uchumi, afya, na maeneo mengine mengi ya kibinadamu.[1]
Nguzo za Uendelevu
haririUendelevu unajengwa juu ya nguzo tatu ambazo ni nguzo ya kijamii, nguzo kwa kimazingira, na nguzo ya kiuchumi.
Uendelevu wa kijamiini unahusiana na hali ya watu. Mfano mmoja ni kulala. Mtu hawezi kuwa na uendelevu kama analala kidogodogo, au sana. Mtu anaweza kuwa na uendelevu kama yeye hulala masaa ya wastani (masaa nane, lakini kila mtu ni tofauti) kila usiku. Kuongeza, kula chakula vizuri ni uendelevu wa kijamiij, kunywa maji safi ni uendelevu wa kijamii, kuwa na marafiki wazuri ni uendelevu wa kijamii.
Uendelevu wa kiuchumi unahusiana na fedha za watu. Mfano mmoja ni benki. Mtu anahitaji pesa kwenye benki hadi anapokuwa mzee. Mtu anahitaji pesa sasa kulipa chakula, nyumba, maji, vitu vya kujiburudisha, kitanda kizuri, na vitu vingine vingi. Kitu kimoja mtu anaweza kufanya kuwa na uendelevu wa kiuchumi ni kutengeneza mipango ya kupata pesa. Mpango mzuri unazingatia kuhusu mapato na matumizi.
Uendelevu wa mazingira ni uendelevu ambao watu wengi wanafikiri kila mara wakati wanaposikia kuhusu uendelevu. Afya ya msitu, afya ya ziwa na mto, afya ya wanyama, na nyingi sana. Mazingira yanaweza kuwa vitu mtu anaishi karibu na. Jengo mtu anajiishi ni mazingira pia. Jengo linahitaji kuwa na safi na amani kuwa na uendelevu.
Kaulimbiu
haririKuna kaulimbiu za uendelevu zinazotumiwa kwa wingi, kama, "Kupunguza, kutumia tena, na kuchakata tena". Kwa ujumla, kitu muhimu sana ni kupunguza ili kuwa na uendelevu. Takataka kidogo ni nzuri kuliko takataka nyingi. Nchi nyingi katika Afrika Mashariki ziliacha kutumia mifuko ya plastiki kupunguza takataka na kuwa na uendelevu.[2] Mara nyingi kupunguza ni kitu cha kwanza kufanywa ili kuwa na uendelevu zaidi. Watu wanaweza kupunguza matumizi ya umeme, muda wa kuoga, gesi chafu, gharama za maisha, na nyingine nyingi.
Mkutano wa Makubaliano (COP)
haririUendelevu wa kimazingira unapata umakini sana kwa sababu ya hali ya dunia. Dunia inapata joto sana, na watu wengi wanaogopa kuhusu hali ya dunia. Watu wengi wanataka kuboresha dunia, lakini watu wengi wanapinga na wengine wanakubaliana kuhusu maoni haya. Umoja wa Mataifa ulitengeneza mipango kumi na saba ya uendelevu. Viongozi wa nchi mbalimbali duniani huzungumza kila miaka kuhusu hali ya dunia na uendelevu katika COP (Mkutano wa Makubaliano). Makubaliano ya kimataifa yanashirikisha nchi za uanachama wa Mkataba wa Kimataifa wa Umoja wa Mataifa, kama Marekani, Burundi, Polandi, na nyingi sana.
Mjadala unakuwa zaidi juu ya uendelevu. Mwanzoni uendelevu ulipopata nafasi ya kimjadala, watu wengi hawakuujali sana. Kadiri muda unavyoendelea, watu wengi wanausadiki, lakini watu wengi wana maoni tofauti kuhusu uendelevu. Mara nyingi, watu wana mabishano kuhusu uendelevu wa kimazingira kwa sababu uendelevu wa kimazingira ni tatizo kubwa sana kwa hali ya dunia. Mara nyingi, COP haifanyi vitu vyingi sana kwa sababu viongozi hawataki kupunguza vitu vyao, kama mafuta, ili kuwa na uendelevu.[3]
Tanbihi
hariri- ↑ University of Pittsburgh. Pitt Sustainability. 2018, Home - Pitt Sustainability. Accessed 17 April 2024
- ↑ Greenpeace Africa. “34 Plastic Bans in Africa | A Reality Check.” Greenpeace, 19 May 2020, 34 Plastic Bans in Africa | A Reality Check - Greenpeace Africa.
- ↑ Bloomberg, AB. (Host). (2021, Nov. 18). We Go Inside the COP26 Climate Talks (No. 67) [Audio podcast episode]. In How to Save a Planet. Gimlet. We Go Inside the COP26 Climate Talks | How to Save a Planet (www.gimletmedia.com)