Ufadhili wa vijana
Ufadhili wa vijana ni neno linalojumlisha mchango wa muda, nguvu au rasilimali, ikiwa ni pamoja na pesa, unaotolewa na watoto na vijana kwa ajili ya shughuli za uhisani. Kulingana na uchunguzi fulani, uhisani wa vijana katika kiwango kikubwa zaidi ni kutoa muda wao, vipaji na hazina zao. Inaonekana kuwa njia nzuri ambayo vijana wanakuza ujuzi na kushiriki katika miradi ya uhisani kama vile kujitolea na huduma za kijamii.
Ufadhili wa vijana huwaelimisha vijana kuhusu mabadiliko ya kijamii ili kutambua matatizo ya jamii na kubuni masuluhisho yafaayo zaidi kwa njia ya kimfumo. Uhisani katika nyanja hii unafafanuliwa kuwa chochote ambacho vijana hufanya ili ulimwengu unaowazunguka uwe mahali pazuri zaidi.
Ukizingatia ushirikiano wa vijana na watu wazima ufadhili wa vijana huwasaidia kukuza ujuzi, maarifa, kujiamini na uwezo wa uongozi. Ufadhili wa vijana pia unatambuliwa kama njia bora ya kuelimisha watoto na vijana kuhusu kujitolea na ushiriki wa kiraia.