Ugonjwa wa Cushing

Ugonjwa wa Cushing (ambao pia unaitwa haipaadrenokotisism au haipakotisism) ni ugonjwa wa homoni (ya mfumo wa mwili) unaosababishwa na viwango vya juu vya kotisoli haipakotisoli katika damu. Hii inaweza kusababishwa na utumizi wa madawa ya glukokortikoidi, au uvimbe unaotoa kotisoli au homoni ya adrenokotikotropiki (ACTH). [1] Ugonjwa wa Cushing unahusu chanzo kimoja maalum, uvimbe (adenoma) katika tezi ya pituitari inayotoa viwango vikubwa vya ACTH, ambayo kwa upande wake huongeza kotisoli. Kwa kawaida unaweza kutibiwa kwa upasuaji. Ulielezwa na Harvey Cushing mwaka wa 1932. [2] [3]

Ugonjwa wa Cushing
Mwainisho na taarifa za nje
Kundi MaalumuEndocrinology Edit this on Wikidata
ICD-10E24.
ICD-9255.0
MedlinePlus000410
eMedicinearticle/117365
MeSHD003480

Dalili za ugonjwa wa Cushing hazipatikani kwa binadamu pekee na bali pia ni hali ya kawaida katika mbwa na farasi waliofugwa.

Ishara na Dalili

hariri

Dalili ni pamoja na kuongeza uzito haraka, hasa wa kiwiliwili na uso na ukiacha viungo (unene wa katikati). Ishara ya kawaida ni ukuaji wa pedi za mafuta ubavuni mwa mtulinga na upande wa nyuma wa shingo (nundu ya nyati) na uso wa duara unaojulikana kama "dalili za wekunduuso". Dalili nyingine ni pamoja na haipahaidrosisi (kutoa jasho jingi kupita kiasi), telangiektasia (mpanuko wa mishipa midogo ya damu), kukonda kwa ngozi (ambako husababisha kuvilia kwa urahisi na kukauka, hasa kwa mikono) na tando zingine za ute, striaeza zambarau au nyekundu (kuongeza uzito katika ugonjwa wa Cushing hunyoosha ngozi, ambayo ni nyembamba na dhaifu, na kuisababisha itoke damu) kwenye kiwiliwili, matako, mikono, miguu au matiti, udhaifu wa misuli ya kupakana (nyonga, mabega), na kuwa na nywele kuruwili (ukuaji wa nywele usoni kwa mfano wa wanaume), na upara na/au kusababisha nywele kuwa kavu mno na nyepesi kukatika. Katika kesi nadra, Cushing inaweza kusababisha idadi ya juu ya kalisi katika damu, ambayo inaweza kusababisha nekrosisi ya ngozi. Kotisoli ya ziada inaweza pia kuathiri mifumo mingine ya endokrini na kusababisha, kwa mfano, kukosa usingizi, kibadilisha-androjeni kilichozuiwa, upungufu wa ashiki, uhanithi, kosa-hedhi / hedhi ya nadra na kutokutungisha kutokana na mwongezeko wa androjeni. Mara kwa mara, wagonjwa hupata mivurugiko mbalimbali ya kisaikolojia , kuanzia furaha hadi kichaa. Unyogovu na wasiwasi pia ni ya kawaida. [4]

Mabadiliko mengine ya kuvutia na ya kudhikisha ya ngozi yanayoweza kuonekana kwenye ugonjwa wa Cushing ni pamoja na chunusi ya uso, wepesi wa kuathirika na maambukizi ya kuvu ngozi na malasezia, ya juu juu, na sifa bainifu ya stria ya atrofi juu ya fumbatio. [5] : 500 

Ishara nyingine ni pamoja na kupita mkojo kupita kiasi (na kiu kisicho cha kawaida kinachoandamana), shinikizo la damu linaloendelea (kutokana na uimarishaji wa athari za kubana mshipa zaepinefrini na kotisoli) upinzani wa insulini (kawaida hasa katika uzalishaji wa ACTH wa ektopia), na hivyo kusababisha haipaglaikemia ( kiwango cha juu cha sukari katika damu) ambayo inaweza kusababisha kisukari melitasi. Ugonjwa wa Cushing usipotibiwa unaweza kusababisha ugonjwa wa moyo na kuongezekakwa vifo. Ugonjwa wa Cushing unaotokana na ACTH ya ziada huweza pia kusababisha kiwango cha juu cha pigmenti, kama vile akanthosi nigrikani katika kwapa. Hii ni kutokana na utengenezaji wa Homoni ya Kudhibiti Rangi ya ngozi kama matokeo ya usanisi wa ACTH kutoka kwa Pro-opiomelanokotini (POMC). Kotisoli pia inaweza kuonyesha shughuli za madinikotikoidi katika viwango vya juu, na kutibua shinikizo la damu na kusababisha kiwango cha chini cha ioni za potasi katika damu (kawaida katika utoaji wa ugiligili wa mwili wa ACTH wa ektopia ). Aidha, usumbufu wa utumbo, maambukizi na uponyaji wa jeraha uliodhoofika (kotisoli ni homoni ya dhiki, kwa hivyo inakandamiza majibu ya kinga na kuvimba). Ugonjwa wa mifupa kuwa midogo na myepesi pia ni hoja katika ugonjwa wa Cushing kwa sababu, kama ilivyotajwa mbeleni, kotisoli huleta jibu linalofanana na mfadhaiko. Kwa hiyo, kukimu kwa mwili ya mfupa (na tishu zingine) hufuata matengenezo ya majibu ya uongo ya dhiki. Zaidi ya hayo, Cushing unaweza kusababisha viunga kuuma na kuwa na mchonyoto, hasa katika nyonga, mabega, na mgongo wa chini.

Sababu

hariri

Kuna mambo kadhaa yanayoweza kusababisha ugonjwa wa Cushing.

Eksojenasi dhidi ya endojenasi

hariri

Homoni kutoka nje ya mwili huitwa eksojenasi, homoni ambazo hutoka ndani ya mwili huitwa endojenasi.

Sababu kuu ya ugonjwa wa Cushing ni kutoa glukokotikoidi , kupitia eksojenesi, zilizoagizwa na tabibu wa huduma ya afya kutibu magonjwa mengine (unaitwa ugonjwa wa Cushing wa iatrojeniki). Hii inaweza kuwa ni madhara ya matibabu ya steroidi ya maradhi mbalimbali kama vile pumu na ugonjwa wa baridi yabisi, au katika uzuiaji wa mwitikio wa kingamwili baada ya kuhamisha kiungo cha mwili. Kutoa ACTH ya kusanisi pia kunawezekana, lakini ACTH haiagizwi mara nyingi kwa sababu ya gharama na matumizi madogo. Ingawa ni nadra, ugonjwa wa Cushing pia unaweza kutokana na matumizi ya medroksiprojesteroni [6] [7]

Ugonjwa wa Cushing wa ndani ya mwili hutokana na uharibifu fulani wa mfumo wa mwili wa kutoa kotisoli. Kwa kawaida, ACTH hutolewa kwenye tezi ya pituitari inapohitajika kuchochea kutolewa kwa kotisoli kutoka kwa tezi za adrena.

  • Katika Cushing ya pituitari, uvimbe hafifu wa pituitari hutoa ACTH. Hii pia hujulikana kama ugonjwa wa Cushing na unahusika katika 65% ya ugonjwa wa Cushing wa ndani ya mwili.
  • Katika Cushing ya adrena, kotisoli hutolewa na uvimbe wa tezi za adrena , tezi za adrena zenye haipaplasia, au tezi za adrena zenye kivimbe cha haipaplasia cha adrena.
  • Hatimaye, uvimbe nje ya mfumo wa kawaida wa pituitari-adrenali unaweza kutoa ACTH inayoathiri tezi za adrena. Etiolijia hii ya mwisho inaitwa Ugonjwa wa Cushing wa ektopia au paraneoplastiki na huonekana katika magonjwa kama saratani ya mapafu ya seli ndogo.

Ugonjwa wa Cushing wa bandia

hariri

Viwango vya juu vya kotisoli jumla vinaweza kusababishwa na estrojini inayopatikana katika dawa za kupanga uzazi zilizo na mchanganyiko wa estrojini na projesteroni. Estrojini inaweza kusababisha ongezeko la kotisoli inayogandisha globulini na hivyo kusababisha jumla ya kiwango cha kotisoli kuongezeka. Hata hivyo, jumla ya kotisoli huria, ambayo ni homoni hai katika mwili, kama ilivyopimwa na mkusanyiko wa mkojo wa masaa 24 kwa kotisoli isio na mkojo, ni kawaida. [8]

Pathofisiolojia

hariri

Haipothalamasi iko katika ubongo na tezi ya pituitari iko chini yake. Kiini kilicho katika ventrikula (PVN) cha haipothalamasi hutoa homoni itoayo tropinigamba (CRH), inayochochea tezi ya pituitari kutoa adrenokotikotropini (ACTH). ACTH husafari kupitia kwenye damu hadi kwa tezi ya adrena, ambapo inachochea kutolewa kwa kotisoli. Kotisoli hutolewa na koteksi ya tezi ya adrena kutoka kwa eneo liitwalo zona fasikulata kama jibu kwa ACTH. Viwango vya juu vya kotisoli huweka majibu hasi kwenye pituitari, ambayo hupunguza kiasi cha ACTH kinachotolewa kutoka kwa tezi ya pituitari. Kwa kweli, dalili za Cushing zinahusu kotisoli ya ziada ya etiolojia yoyote. Sababu moja ya dalili za Cushing ni uvimbe unaotoa kotisoli katika koteksi ya tezi ya adrena. Uvimbe husababisha vinwango vya kotisoli katika damu kuwa vya juu sana, na majibu hasi kwenye pituitari kutoka kwa viwango vya juu vya kotisoli husababisha viwango vya ACTH kuwa vya chini sana. Ugonjwa wa Cushing unahusu tu haipakotisoli inayofuata sekondari katika utoaji wa ziada wa ACTH kutoka kwa uvimbe wa kotikotrofia wa pituitari. Hii husababisha viwango vya ACTH kwenye damu kuongezeka pamoja na kotisoli kutoka kwa tezi ya adrena. Viwango vya ACTH vinasalia vya juu kwa sababu uvimbe huifanya pituitari kutovutiwa na majibu hasi kutoka kwa viwango vya juu vya kotisoli.

Ugonjwa wa Cushing pia ulikuwa ugonjwa wa kwanza wa kingamwilinafsi kutambuliwa kwa binadamu. [9]

Uaguzi

hariri

Wakati dalili za ugonjwa wa Cushing zinatuhumiwa, ama uchunguzi wa ukandamizaji wa deksamethasoni (utoaji wa deksamethasoni na utambuzi wa mara kwa mara wa kotisoli na kiwango cha ACTH), au kipimo cha kotisoli kwenye mkojo kwa masaa 24 hutoa viwango sawa vya ugunduzi. [10] Deksamethasoni ni glukokotikoidi na inaiga madhara ya kotisoli, ikiwa ni pamoja na majibu hasi kwenye tezi ya pituitari. Wakati deksamethasoni inapotolewa na sampuli ya damu inachunguzwa, kotisoli ya juu inaashiria dalili za Cushing kwa sababu kuna chanzo cha ektopia cha kotisoli au ACTH (mfano: uvimbe wa adrena)ambayo haizuiwi na deksamethasoni. Mtazamo mpya, uliokubaliwa hivi karibuni na FDA (Utawala wa Vyakula na Madawa ulio chini ya wizara ya Afya ya Marekani. Jukumu lake ni kulinda na kukuza afya ya umma kwa kuratibisha na kusimamia uslama wa vyakula na madawa) ya Marekani, ni uchunguzi wa kotisoli katika mate kwa masaa 24, ambayo pia inaweza kuwa nyeti, kwa vile viwango vya usiku vya kotisoli ya mate ya wagonjwa wenye Cushing ni vya juu. Viwango vingine vya homoni ya pituitari vitahakikishwa. Uchunguzi wa kimwili kutambua dosari yoyote ya eneo la kuona utahitajika ikiwa kidonda cha pituitari kinatuhumiwa. Kidonda hiki kinaweza kubana mahali ambapo neva za macho hukutana na kusababisha hemianopsia ya kawaida ya macho.

Wakati wowote wa ambapo uchunguzi huu ni halisi, skani ya CT ya tezi ya adrena na MRI ya tezi ya pituitari hufanywa kuchunguza kuwepo na uvimbe au insidentaloma (ugunduzi wa dharura wa vidonda visivyo vya kudhuru) ya adreni au pituitari. Sintigrafia ya tezi ya adreni kwa skani ya ayodokolesteroli ni muhimu mara kwa mara. Mara chache sana, kuamua viwango vya kotisoli katika vena mbalimbali katika mwili kwa kupima vena kutumia katheta, ukielekea kwenye pituitari (uchunguzi wa uwazi katika mfupa mwambo)ni lazima.

Nemoniki

hariri

K - unene wa K katikati, pedi nene za K kizazi, udhaifu wa unyuzi wa K olajeni , K omedoni (chunusi)
U - Kotisoli isio na mkojo na ongezeko la glukosi
S - Stria, kinga iliyokandamizwa
H - Haipakotisoli, Shinikizo la damu, Haipaglaikemia, Kuwepo kwa nywele nyingi kupita kiasi kwenye mwili na uso
I - Iatrojeniki (Ongezeko la utoaji wa steroidi za bongo)
N - Noniatrojeniki (Neoplasmi)
G - Kutostahimili glukosi, Kudumaa kwa ukuaji

Matibabu

hariri

Visa vingi vya ugonjwa wa Cushing vinasababishwa na matibabu ya steroidi (iatrojeniki). Kwa hiyo, wagonjwa wengi hutibiwa kwa ufanisi kwa kupunguza taratibu (na hatimaye kuacha) madawa ambayo husababisha dalili.

Kama uvimbe wa adrena utatambuliwa unaweza kuondolewa kwa upasuaji. Uvimbe wa kotikotrofia wa pitituari unaotoa ACTH unapaswa kuondolewa baada ya utambuzi. Bila kutia maanani eneo la uvimbe, wagonjwa wengi watahitaji ubadili wa steroidi baada ya uppasuaji angalau kwa muda kwa sababu ukandamizaji wa muda mrefu wa ACTH ya pituitari na tishu ya kawaida ya adrena hauponi mara moja. Hakika, ikiwa adrena zote mbili zitaondolewa, kuleta haidrokotisoni au prinisolonibadala yake ni muhimu.

Kwa wale wagonjwa ambao hawafai au wasiotaka kufanyiwa upasuaji, madawa kadhaa yamepatikana kuzuia usanisi wa kotisoli (km ketokonazoli, metiraponi) lakini ni ya utendakazi mdogo.

Kuondolewa kwa adrena pasipo na uvimbe unaojulikana hutekelezwa mara kwa mara ili kuondosha utoaji wa kotisoli ya ziada. Wakati mwingine, hii huondoa majibu hasi kutoka kwa uvimbe wa pituitari uliokuwa umejificha hapo mbeleni, unaoanza kukua kwa haraka na kutoa viwango vikubwa mno vya ACTH, na hivyo kusababisha kiwango cha juu cha pigmenti, hasa kwenye ngozi. Hali hii ya kiafya inajulikana kama ugonjwa wa Nelson. [11]

Epidemiolojia

hariri

Ugonjwa wa Cushing wa iatrojeniki (unaosababishwa na matibabu kwa kutumia steroidi za bongo) ni aina ya kawaida kupita zote ya ugonjwa wa Cushing. Matukio ya uvimbe wa pituitari yanaweza kuwa mengi, kama vile kwa mtu mmoja kati ya watano, [12] lakini sehemu ndogo tu ndio tenda-kazi na huzalisha homoni nyingi zaidi.

Watu wazima wenye ugonjwa huo pia wanaweza kuwa na dalili ya kuongeza uzito kuzidi kiasi, ukuaji wa nywele kupita kiasi kwa wanawake, shinikizo la damu, na matatizo ya ngozi. Aidha, wanaweza kuonyesha:

  • udhaifu wa misuli na mifupa
  • usununu, kuwashwa, au unyogovu
  • kutatizika kwa usingizi
  • kiwango cha juu cha sukari
  • maradhi ya hedhi kwa wanawake na upungufu wa uwezo wa kuzaa kwa wanaume
  • upara
  • kiwango cha juu cha kolesteroli katika damu

Marejeo

hariri
  1. Kumar, Abbas, Fausto. Msingi wa Patholojia wa Magonjwa wa Robbins na Cotran, toleo la 7. Elsevier-Saunders, New York, 2005.
  2. Cushing HW. (1932). "The basophil adenomas of the pituitary body and their clinical manifestations (pituitary basophilism)". Bulletin of the Johns Hopkins Hospital. 50: 137–95.
  3. "Dr. Cushing Dead; Brain Surgeon, 70. A Pioneer Who Won Fame as Founder of New School of Neuro-Surgery. Discovered Malady Affecting Pituitary Gland. Was Noted Teacher and Author", New York Times, 8 Oktoba 1939. Retrieved on 2010-03-21. "Dr. Harvey Williams Cushing, international authority on brain surgery and neurology, who for his ..." 
  4. Yudofsky, Stuart C. (2007). The American Psychiatric Publishing Textbook of Neuropsychiatry and Behavioral Neurosciences (tol. la 5th). American Psychiatric Pub, Inc. ISBN 1585622397. {{cite book}}: Unknown parameter |coauthors= ignored (|author= suggested) (help)
  5. James, William, Berger, Timotheo, Elston, Dirk (2005). Magonjwa ya Ngozi ya Andrews: Elimu ya ngozi ya kiafya. (10 ed).. Saunders. ISBN 0-7216-2921-0.
  6. http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/2552887
  7. http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pubmed/2144198
  8. http://www.ncbi.nlm.nih.gov/pmc/articles/PMC1436049/
  9. [13] ^ Historia ya Ugonjwa wa Cushing: hadithi ya utata, JR Soc Med. 1991 Juni, 84 (6): 363-366
  10. Raff H, Findling JW (2003). "A physiologic approach to diagnosis of the Cushing syndrome". Ann. Intern. Med. 138 (12): 980–91. PMID 12809455.
  11. Nelson DH, Meakin JW, Thorn GW (1960). "ACTH-producing pituitary tumors following adrenalectomy for Cushing syndrome". Ann. Intern. Med. 52: 560–9. PMID 14426442.{{cite journal}}: CS1 maint: multiple names: authors list (link)
  12. Ezzat S, Asa SL, Couldwell WT; na wenz. (2004). "The prevalence of pituitary adenomas: a systematic review". Cancer. 101 (3): 613–9. doi:10.1002/cncr.20412. PMID 15274075. {{cite journal}}: Explicit use of et al. in: |author= (help)CS1 maint: multiple names: authors list (link)

Viungo vya nje

hariri