Hadimu

(Elekezwa kutoka Uhadimu)

Kuhusu wakazi wa maeneo ya kisiwani Unguja angalia hapa Wahadimu

Hadimu ni mtu anayepaswa kumhudumia mwingine kutokana na hali yake katika jamii. Mahadimu ni tofauti na watu huru lakini pia tofauti na watumwa.

Katika jamii ya Afrika ya Mashariki mahadimu walikuwa watumwa waliopewa uhuru na watoto wao waliotakiwa bado kutoa huduma fulani kwa mabwana wa awali au familia yake. Wahadimu wa Unguja wana historia tofauti.

Katika makala hii istilahi “hadimu” inatumiwa pia kutaja watu walioitwa kwa Kiingerezaserf” au “indentured servant” yaani watu waliopaswa kufanya kazi kwa watu wengine isiyo ya hiari. Mahadimu kwa maana hiyo waliweza kuzaliwa hivyo na kulazimishwa kuwa mahadimu maisha yao yote pamoja na watoto wao. Lakini kulikuwa pia na taratibu ambapo uhadimu uliendelea kwa kipindi cha miaka kadhaa pekee.

Hata kama mahadimu walikuwa tofauti na watumwa, wakati mwingine si rahisi kuona tofauti hiyo, maana taratibu za uhadimu mkali na utumwa mpole ziliweza kufanana. Tabia ya pamoja ni kazi ya kulazimishwa kwa kumtegemea bwana maalumu juu yao pamoja na kukosa haki zinazokubaliwa kwa watu wote walio huru.