Ukatili wa kimwili

aina ya unyanyasaji unaoonyeshwa na mtu kumdhuru mtu mwingine kimakusudi

Ukatili wa kimwili ni matendo ambayo yanaweza kumsababishia mtu maumivu na majeraha katika akili, mwili, au matendo ambayo yanaweza kumsababishia mtu mateso kwa njia yoyote ile. Matendo ya ukatili wa kimwili yanaweza kufanywa na mtu mmoja dhidi ya mtu mwingine.

Watoto wamekuwa sehemu ya wahanga wakubwa wa matendo ya ukatili wa kimwili, kama ulivyo ukatili wa majumbani, na wakati mwingine ukatili wa kimwili huweza kupeleka mtu kuaga Dunia.

Visababishi hariri

Mara nyingi watoto wamekuwa wakikumbana na vitendo vya ukatili wa kimwili kutoka kwa wazazi wao kutokana na adhabu wanazozipata.[1][2] Matukio mengi ya ukatili wa kimwili yamekuwa na sababu mbalimbali ikiwemo hali ya mazingira katika familia, msongo wa mawazo, pamoja na kukosekana uelewa.

Marejeo hariri

  1. "Child physical abuse". American Humane Association.
  2. Giardino, A.P.; Giardino, E.R. (12 December 2008). "Child Abuse & Neglect: Physical Abuse". WebMD.
  Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Ukatili wa kimwili kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.