Ukoma
Ukoma (pia ugonjwa wa Hansen; kwa Kiingereza: leprosy) ni ugonjwa wa kuambukiza wa kudumu unaosababishwa na bakteria Mycobacterium leprae na M. lepromatosis [1] [2].
Ukoma | |
---|---|
Mwainisho na taarifa za nje | |
Kundi Maalumu | Infectious disease |
ICD-10 | A30. |
ICD-9 | 030 |
OMIM | 246300 |
DiseasesDB | 8478 |
MedlinePlus | 001347 |
eMedicine | med/1281 derm/223 neuro/187 |
MeSH | D007918 |
Baada ya ambukizo kuna kipindi ambapo mgonjwa hana dalili za ukoma. Kipindi hicho bila dalili kinaweza kuendelea hadi miaka 5 au hata miaka 20[2]. Dalili zinazoonekana ni kwa mfano vidonge vya chembe vya neva, vya mfumo wa upumuaji, vya ngozi na vya macho [2].
Wakati dalili zinapoanza kuonekana mgonjwa hasikii tena baridi, joto wala maumivu. Kwa hiyo hatambui kirahisi kama amepata jeraha. Vidonda vinavyotokea haviumi na uchafu pamoja na bakteria hatari zinaingia mwilini. Hivyo vidonda vinaweza kuwa vikubwa zaidi kwa sababu havitibiwi au vinachelewa kutibiwa. Ndiyo sababu pengine wakoma wanapotea viungo vya mwili kama vidole na hata mguu au mkono kutokana na majeruhi yanayorudiarudia.[3]
Udhaifu pamoja na macho kutoona vyema pia yanamwathiri mgonjwa.[3]
Uaguaji
haririAina mbili za maradhi zinatambulika kutokana na idadi ya bakteria zilizopo: “paucibacillary” na “multibacillary.”[3] Aina hizo mbili zinatofautishwa na kiasi cha alama zenye ganzi, na “hypopigmintation” ukosefu wa rangi ngozini, huku hali ya “paucibacillary” kuwa na kiasi kisichozidi tano, hali ya “multibacillary” kuwa na zaidi ya tano. [3]
Uaguaji unathibitishwa na “acid-fast bacilli” kuwepo katika biopsi ya ngozi au kutokana na utambulisho wa DNA kwa “polymerase chain reaction”.[3]
Maradhi hayo hutokea zaidi miongoni mwa watu maskini yanaaminika kuambukiza kwa kupelekwa na matone ya upumuo. [3] Ukali wake kuambukiza ni ndogo.[3]
Matibabu na uenezi
haririUkoma unapona kutokana na matibabu.[2] Ukoma wa “paucibacillary” unatibika kwa dawa za “dapsone” na “rifampicin” kwa muda wa miezi 6.[3] Ukoma wa “multibacillary” unatibika kwa dawa za “rifampicin”, “dapsone”, na “clofazimine” kwa muda wa miezi 12.[3] Shirika la Afya Duniani[2] hutoa dawa hizo bure. Baadhi ya antibiotiki zinaweza kutumika.
Katika dunia nzima mwaka wa 2012, idadi ya wagonjwa wa ukoma wa muda mrefu ilikuwa 189,000 huku idadi ya wagonjwa waliougua katika muda mfupi wa mwaka huo ilikuwa 230,000.[2][4] Idadi ya wagonjwa waliokuwa na ukoma kwa muda mrefu ilipunguka kutoka takriban milioni 5.2 kwenye miaka ya 1980.[2][4][5]
Takriban wagonjwa wote wapya wanaishi katika nchi 16, India ikiwa na zaidi ya nusu ya wakoma wote.[3]
Katika muda wa miaka 20, milioni 16 katika dunia nzima walipona ukoma.
Historia, jamii, na utamaduni
haririUkoma umeathiri binadamu tangu miaka elfu nyingi zilizopita.[3] Maradhi hayo yamepata jina lake kutoka neno la Kilatini lepra, maana yake ni mwenye gamba kwenye ngozi. Jina la “maradhi ya Hansen” linatokana na jina la daktari Gerhard Armauer Hansen.[3] [6]
Unyanyapaa
haririKutenga wagonjwa katika makambi ya wakoma bado kunatokea. Katika nchi kama India makambi hayo yapata zaidi ya elfu. Pia China[7] [8] [8] yako yapata mia kadhaa, na Afrika. Hata hivyo, takriban makambi yote yamefungwa. Ukoma umewatambulisha wagonjwa wake kubaguliwa tangu muda wa karibu historia yote uliyo nayo ugonjwa. Ubaguzi huo bado ni kizuio cha fedheha ambacho kinahamasisha wagonjwa kujificha na kukosa matibabu mapema.
“Siku ya Ukoma Duniani” ilianzishwa mwaka wa 1954 kuwatambulisha wagonjwa hao wafahamike na kujulikana kama binadamu wanaostahili heshima na fursa ya kuchangia jamii kwa vipaji vyao.[9]
Marejeo
hariri- ↑ <name=New2008>"New Leprosy Bacterium: Scientists Use Genetic Fingerprint To Nail 'Killing Organism'". ScienceDaily. 2008-11-28. Iliwekwa mnamo 2010-01-31.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 2.6 "Leprosy Fact sheet N°101". World Health Organization. Jan 2014.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) Hitilafu ya kutaja: Invalid<ref>
tag; name "WHO2014" defined multiple times with different content - ↑ 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 3.10 3.11 Suzuki K, Akama T, Kawashima A, Yoshihara A, Yotsu RR, Ishii N (Februari 2012). "Current status of leprosy: epidemiology, basic science and clinical perspectives". The Journal of dermatology. 39 (2): 121–9. doi:10.1111/j.1346-8138.2011.01370.x. PMID 21973237.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) CS1 maint: multiple names: authors list (link) - ↑ 4.0 4.1 "Global leprosy situation, 2012". Wkly. Epidemiol. Rec. 87 (34): 317–28. Agosti 2012. PMID 22919737.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Rodrigues LC, Lockwood DNj (Juni 2011). "Leprosy now: epidemiology, progress, challenges, and research gaps". The Lancet infectious diseases. 11 (6): 464–70. doi:10.1016/S1473-3099(11)70006-8. PMID 21616456.
{{cite journal}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Walsh F. "The hidden suffering of India's lepers", BBC News, 2007-03-31.
- ↑ Lyn TE. "Ignorance breeds leper colonies in China", Independat News & Media, 2006-09-13. Retrieved on 2010-01-31. Archived from the original on 2010-04-08.
- ↑ 8.0 8.1 Byrne, Joseph P. (2008). Encyclopedia of pestilence, pandemics, and plagues. Westport, Conn.[u.a.]: Greenwood Press. uk. 351. ISBN 9780313341021.
- ↑ McMenamin, Dorothy (2011). Leprosy and stigma in the South Pacific : a region-by-region history with first person accounts. Jefferson, N.C.: McFarland. uk. 17. ISBN 9780786463237.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |