Ulaya ya Magharibi

Ulaya ya Magharibi ni sehemu ya magharibi ya bara la Ulaya. Kuna maelezo ya kutofautiana ni nchi zipi ambazo ni sehemu ya kanda hili. Maelezo hutofautiana kutokana na njia mbalimbali za kuangalia sehemu hiyo: kwa maana ya kijiografia, kihistoria, kisiasa au kiutamaduni.

Ulaya ya Magharibi kijiografia kufuatana na CIA-Factbook (njano); njano nyeupe: Ulaya ya Kusini-Magharibi

Kanda la kijiografiaEdit

Kama kanda la kijiografia ni mara nyingi nchi zifuatazo zinazohesabiwa kuwa Ulaya ya Magharibi:

 
Ulaya ya Magharibi kufuatana na mpangilio wa Umoja wa Mataifa (buluu nyeupe);
Buluu nyeusi: Ulaya ya Kaskazini
Kijani: Ulaya ya Kusini
Nyekundu: Ulaya ya Mashariki

Mpangilio wa Umoja wa MataifaEdit

Umoja wa Mataifa umepanga kanda hili tofauti hasa kwa kuhesabu Ufalme wa Muungano upande wa Ulaya ya Kaskazini lakini kuingiza Ujerumani, Austria na Uswisi ambazo zinahesabiwa mara nyingi kama sehemu ya Ulaya ya Kati; ila tu mpangilio wa UM hauna Ulaya ya Kati.

 
Ulaya ya Magharibi kisiasa wakati wa Vita Baridi
Buluu: Ulaya ya Magharibi (NATO)
Kijivu: Nchi zisizofungamana na upande wowote
Nyekundu: Ulaya ya Mashariki (upande wa Umoja wa Kisovyeti)

Ulaya ya Magharibi kihistoria katika karne ya 20Edit

Wakati wa "vita baridi" Ulaya ya Magharibi ilimaanisha mara nyingi nchi zote za Ulaya zilizofungamana na upande wa magharibi yaani Marekani na NATO dhidi nchi za kikomunisti zilizoshikamana na Umoja wa Kisovyeti.