Umoja wa Muungano wa Afrika
Umoja wa Muungano wa Afrika (Kiingereza: Organisation of African Unity, OAU; Kifaransa: Organisation de l'Unité Africaine, OUA) ulikuwa jumuiya ya nchi huru za Afrika iliyoanzishwa 1963 na kudumu hadi 2002. Ulikuwa mtangulizi wa Umoja wa Afrika ambao ni jumuiya ya nchi za Afrika tangu Julai 2002.
OAU iliundwa tarehe 25 Mei 1963 mjini Addis Abeba na nchi 30 za Afrika. Kwenye mkutano wa 11 Julai 2001 Mkutano Mkuu uliamua kuunda Umoja wa Afrika kama haua mpya kwenye harakati ya kuungana Afrika na OAU ilifungwa tar. 9 Julai 2002.
Mwishoni nchi zote za Afrika zilikuwa wanachama isipokuwa Moroko iliyojitenga mwaka 1985 baada ya Sahara ya Magharibi kupokelewa katika OAU.