Unanswered Prayers
"Unanswered Prayers" ni wimbo ambao ulitolewa na kuandikwa na msanii wa Muziki wa Country wa Marekani Garth Brooks ambao ulifika #1 katika chati za country billboard za 1990. Ulianza kama debut katika albamu ya No Fences na pia unaonekana katika albamu za The Hits, The Limited Series, na Double Live. Uliandikwa na Brooks, Pat Alger na Larry Bastian.
“Unanswered Prayers” | ||
---|---|---|
Single ya Garth Brooks | ||
B-side | "Alabama Clay" | |
Imetolewa | Oktoba 1990[1] | |
Mtunzi | Pat Alger Larry Bastian Garth Brooks |
"Unanswered Prayers" ni moja kati ya rekodi maarufu zaidi za Brook na ni moja ya vibao mashughuli vilivyosaidia albamu yake ya "No Fences" kukaa uongozini mwa chati kwa miezi mingi (zaidi ya wiki 30 katika nafasi ya 1 katika chati za Billboard Country). Katika tamasha, mashabiki huimba pamoja neno baada ya neno jinsi inavyoonekana katika "Double Live" (1998) ya Brook.
Wimbo
hariri- Key: D Major
- Urefu: 3:23
Katika "Unanswered Prayers," mwanaume anakutana na mpenziwe wa shule katika mji wa nyumbani wakati wa mechi ya Soka. Anapojitambulisha kwake anakumbuka uhusiano wao wa awali na jinsi alivyokuwa ameomba kuwa msichana huyu angekuwa wake wa maisha. Anagundua kuwa wote wawili wamebadilika halafu anamwangalia mkewe na kugundua kuwa Mungu Alijua Alikuwa Anafanya nini wakati huu wote:
- Sometimes I thank God for unanswered prayers
- Remember when you're talking to the man upstairs
- That just because he doesn't answer doesn't mean he don't care
- Some of God's greatest gifts are unanswered prayers
(
- Saa zingine ninamshukuru Mungu kwa maombi ambayo hakujibu
- Kumbuka ukiongea na aliye juu
- Kuwa kwa kuwa hakuyajibu maombi yako
Haimaanishi hakujali
- Baadhi ya zawadi kuu za Mungu ni Maombi yasiyojibiwa
)
Kulingana na Garth, wimbo huu unaangazia hali ya ukweli;
" unanswered Prayers ilikuwa hisia za moyo wangu abazo nilizimwaga kwa wimbo huu. Ni tukio la ukweli lililontendekea na Sandy. Mnamo Oktoba 1989, niliona ua langu la nyakati za shule. Ninaweza kusema sasa ingawa sikuwahi kusema: Katika miaka ya kwanza miwili ya ndoa yangu, bado nilikuwa nikifikiria kuwa msichana huyo ndiye niliyefaa kumwoa. Lakini sasa unapong’amua kuwa ulicho nacho ndicho bora zaidi ungepata, inakufanya ulale kwa amani"[2]. Katika vidokezo vya mistari ya kuanzia ya albamu ya "The Hits" ya 11994, Brooks ananukuliwa akisema, “kila mara nikliimba wimbo huu hunipafunzo lile lile: Raha haihusiani na kupata ukitakacho, ni kukitaka kile ulicho nacho”.
Nafasi katika Chati
haririChati (1990-1991) | Kilele |
---|---|
U.S. Billboard Hot Country Singles & Tracks | 1 |
Canadian RPM Country Tracks | 1 |
Matoleo Mengine
haririPat Alger, Mtunzi msaidizi katika wimbo huu, alirekodi toleo lake la "Unanswered Prayers" mnamo 1994. Ilishirikishwa kama kibao cha kufungia katika albamu yake ya Seeds.
Viejeleo
hariri- ↑ Garth Brooks singles at LP Discography.com link
- ↑ "Transcription from "The Garth Brooks Story" (1995)". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2009-04-14. Iliwekwa mnamo 2010-01-21.
Viungo vya nje
hariri- "Unanswered Prayers" Lyrics Ilihifadhiwa 24 Machi 2010 kwenye Wayback Machine.
Alitanguliwa na "I've Come to Expect It From You" ya George Strait |
Billboard Hot Country Singles & Tracks Single ya Kwanza 12 Januari- 19 Januari 1991 |
Akafuatiwa na "Forever's as Far as I'll Go" ya Alabama |
RPM Country Tracks Single ya Kwanza 26 Januari-2 Februari 1991 |
Akafuatiwa na "Rumor Has It" ya Reba McEntire |