Underclassman

Underclassman ni filamu ya mwaka wa 2005 ambamo ndani yake ina mapigano na vichekesho. Filamu imeongozwa na Marcos Siega, na waigizaji wake ni Nick Cannon, Shawn Ashmore, Roselyn Sánchez, Kelly Hu, Hugh Bonneville, na Cheech Marin. Filamu ilitolewa mnamo tar. 2 Septemba 2005, awali ilipanga itolewe kunako mwaka wa 2004.

Underclassman
Underclassman film.jpg
Theatrical release poster
Imeongozwa na Marcos Siega
Imetayarishwa na Peter Abrams
Robert L. Levy
Andrew Panay
Imetungwa na Brent Goldberg
David Wagner
Nyota Nick Cannon
Shawn Ashmore
Roselyn Sánchez
Kelly Hu
Hugh Bonneville
Cheech Marin
Muziki na BT
Imehaririwa na Nicholas C. Smith
Imesambazwa na Miramax Films
Imetolewa tar. Septemba 2, 2005 (2005-09-02)
Ina muda wa dk. 95 minutes
Nchi Marekani
Lugha Kiingereza
Mapato yote ya filamu $5,655,459

HadithiEdit

Tracy (Trey) Stokes (Cannon) ni askari kanzu mwenye umri wa miaka 23-ambaye ametumwa kwenda kuchunguza kifo cha mwanafunzi wa shule ya Westbury High. Amekuja kuwa rafiki na Rob Donovan (Ashmore) na punde anagundua kama jamaa ana kawaida ya kuiba magari kwenye sherehe.

Karibia na mwisho, inagundulika kwamba mkuu wa shule (Bonneville) alikuwa akimtisha Donovan, na ndiye alikuwa mratibu mkuu wa uhalifu. Baada ya kupigwa chini kikosini na mkuu wa polisi (Marin), Trey ameweza kusaidia kesi kwisha (kwa msaada wa Donovan) na akarejeshwa kazini.

WashirikiEdit

MapokeoEdit

Underclassman imepokea tahakiki mbovu kabisa kutoka kwa watahakiki. Kwenye Rotten Tomatoes, watahakiki wameipa 6%.[1]

MarejeoEdit

  1. Underclassman (2004). Rotten Tomatoes (2010-07-08). Iliwekwa mnamo 2010-07-08.

Viungo vya njeEdit

  Makala hii kuhusu filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Underclassman kama waigizaji wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.