Umoja, Sudan Kusini

(Elekezwa kutoka Unity, Sudan)

Coordinates: 9°0′N 29°42′E / 9.000°N 29.700°E / 9.000; 29.700


Umoja (Kar. الوحدة al-wahda) ni moja ya majimbo ("wilayat") ya Sudan Kusini. Awali lilikuwa na ukubwa wa eneo la Km² 22,122 na wakazi 4,700,000 (2000). Bentiu ulikuwa ndio mji mkuu wa jimbo hili lenye wilaya tisa na ambalo ni eneo la mafuta baadhi ya mashamba yenye utajiri mkubwa wa mafuta.

Unity (Wahda)

Wakati serikali ya Sudan mjini Khartoum ilitambua jina la Alwahda = Umoja, serikali mpya ya Sudan Kusini ilitambua jimbo hili kama Nile ya juu ya Magharibi (Western Upper Nile). Kabla ya mpangilio wa kiutawala wa mwaka wa 1994, Umoja ilikuwa sehemu ya jimbo kubwa la Upper Nile.

Umoja ilikaliwa na makabila mawili, ya Nuer (wengi) na Dinka (wachache). Kama majimbo mengine ya Sudan Kusini, jimbo la Umoja linajumuisha wilaya saba: Mayom, Rubkona, Leer, Guit, Koch, Mayiandit na Payinjiar.

Wilaya za Abeimnom na Parieng zilitengwa na jimbo na kuwa eneo maalum ya kiutawala la Ruweng.

Uchumi hariri

Kilimo ndio shughuli ya kiuchumi ya msingi katika jimbo hili. Watu ni wafugaji wahamaji ambao hujihusisha na kilimo na ugygaji, hasa ng'ombe. Kilimo hufanywa wakati wa msimu wa mvua ingawa baadhi ya ukulima pia hufanywa wakati wa majira ya joto. Mboga hazilimwi sana kwani wakulima wengi huishi vijijini kuliko mijini, na hivyo kukosa kupata masoko kwa mazao yao. Baadhi ya Mashirika Yasiyo ya Kiserikali inawahamasisha wakulima kuanzisha utaratibu wa kilimo kwa ajili ya soko.

Uwanja wa Mafuta wa Unity hariri

Mafuta ya petroli ya kwanza ya Sudan iligunduliwa Umoja mwaka wa 1970. Makampuni ya mafuta ya kimataifa ambazo zinahusika katika kupeleleza mafuta katika Umoja zilichangia pakubwa kupoteza makaazi ya wakazi wazawa. [1]

Kiwanja cha mafuta cha Umoja kinapatikana ndani ya mgodi mkubwa wenye madini aina ya hydrocarbon katika bonde la ufa la Muglad na kina kadiriwa kuwa na mapipa milioni 150 ya mafuta. [2] Bomba Kubwa la Mafuta la Nile huanzia katika kiwanja cha mafuta cha Unity.

Marejeo hariri

  1. Human Rights Watch , 'Sudan, oil, and human rights', www.hrw.org , Novemba.
  2. NPA Group 2008, 'Sudan - Muglad Basin' Archived 17 Mei 2008 at the Wayback Machine., www.npagroup.co.uk , 27 Februari. Retrieved on 5 Machi 2008.

Viungo vya nje hariri