Usimilishaji ni jinsi watu kutoka utamaduni au kabila dogo hufanywa kuwa na mila na kuzichukua tamaduni za kabila kubwa au inayotawala. Watu waliosimilishwa kikamilifu hukosa sifa za kuwatofautisha ila tu kimwili.

Usimilishaji unaweza kufanyika kwa kutumia nguvu au kutumia mambo ya kitamaduni, k.v. ndoa za kabila tofauti[1][2].

Hata hivyo mara nyingine mchakato huo unatokana na hiari ya watu wanaopenda utamaduni wa kigeni na kuuiga hata kupotewa na utambulisho wao.

Mifano Edit

Usimilishaji wa Wadorobo na Ogiek Edit

Wadorobo wanajulikana kuwa watu wa kwanza kuishi Kenya. Waliishi katika Bonde la Ufa na katikati ya Kenya. Wamasai, Wanandi, Wakipsigis na Wakikuyu walihamia huko na kupanua mipaka katika maeneo waliyokuwa wakiishi Wadorobo nao walichukua mila na lugha za makabila makubwa yaliyoishi karibu nao[3].

Usimilishaji katika makoloni ya Ufaransa Edit

Itikadi ya Ufaransa kutawala makoloni yake ilikuwa usimilishaji. Watawaliwa walitakiwa kujifunza mila na utamaduni wa Wafaransa. Walipewa uraia wa Ufaransa na haki na majukumu yote ya raia wa Ufaransa bila kujalisha hadhi au rangi. Itikadi hiyo ilikubaliana na nadharia tawala ya Ufaransa, Liberté, égalité, fraternité (Uhuru, usawa, undugu)[4].

Marejeo Edit

  1. "Assimilation | society", Encyclopedia Britannica (in English), retrieved 2018-08-04 
  2. "Cultural Assimilation: Meaning and Examples for Better Clarity", Historyplex (in en-US), retrieved 2018-08-04 
  3. "The Dorobo Peoples of Kenya and Tanzania Archived 29 Julai 2018 at the Wayback Machine.", iliwekwa mnamo 04/08/2018
  4. Idowu, H. Oludare (1969). "Assimilation in 19th Century Senegal" (in fr-FR). Cahiers d’études africaines 9 (34): 194–218. doi:10.3406/cea.1969.3162 . ISSN 0008-0055 . https://www.persee.fr/doc/cea_0008-0055_1969_num_9_34_3162.