Utando wa seli ni rusu nyembamba kama ngozi inayopakana seli za viumbehai. Majina ya Kiingereza ni cell membrane, plasma membrane au cytoplasmic membrane.

Utando wa seli (extracellular: Nje ya seli; Lumen of cell: Ndani ya seli; hydrophilic: ya kukubali maji; hydrophobic: ya kukataza maji)

Kazi yake ni kutenganisha ndani na nje, yaani yaliyomo ya seli na na yale yalio nje yake.[1][2]

Kwa kila seli ni muhimu kukinga na kutenganisha plasma iliyopo ndani yake na athira au kemikali za nje. Seli za wanyama zinatenganishwa kati yao na utando wa seli pekee.

Kwenye seli za mimea, fungi na bakteria kuna pia ukuta wa seli nje ya utando. Ukuta wa seli (ing. cell wall) unaimarisha seli, unaongeza kinga na kuwa kama filta dhidi ya molekuli kubwa.

Utando wa seli unafanywa na safu mbili za molekuli zinazoitwa "fosfo-lipidi". Maana yake molekuli hizi zina sehemu ya fosfati upande mmoja na sehemu ya lipidi (mafuta) upande mwingine. Upande wa kifosfati inachanganya na maji lakini sehemu ya kimafuta inakataa maji. Kuna pia proteini nyingine zinazoweza kuongezwa ndani ya utando. Kwa njia hii seli inaweza kutawala ni nini inayoweza kuingia au kutoka.


Marejeo

hariri
  1. Kimball's biology pages Ilihifadhiwa 25 Januari 2009 kwenye Wayback Machine., Cell membranes
  2. Singleton P, (1999). Bacteria in biology, biotechnology and medicine (tol. la 5th). New York: Wiley. ISBN 0-471-98880-4.{{cite book}}: CS1 maint: extra punctuation (link)