Utumbo mpana (kwa Kiingereza large intestine) ni sehemu ya utumbo kati ya utumbo mwembamba na mkundu. Hivyo unapatikana karibu na mwisho wa mfumo wa mmeng'enyo wa chakula.

Sehemu za utumbo mpana: 1. Sikamu (caecum) na kibole (appendix), 2. utumbo mpana wa kupanda (ascending colon), 3. utumbo mpana wa kulala (transverse colon), 4. utumbo mpana wa kutelemka (descending colon), 5. utumbo mpana wa sigma (sigmoid colon), puru (rectum), mkundu (anus)

Kazi ya utumbo mpana

hariri

Chakula kinachotoka katika utumbo mwembamba na kuingia utumbo mpana huwa ni kile ambacho hakikuweza kumeng’enywa au kile ambacho kimeng’enywa lakini hakikusharabiwa. Sehemu ndogo tu ya chakula kilichomeng’enywa husharabiwa na utumbo mpana. Sehemu kubwa ya maji iliyotokana na mmeng’enyo wa chakula husharabiwa na utumbo mpana. Sehemu iliyobaki ya chakula huelekea kwenye rektamu na kutolewa nje kupitia njia ya haja kubwa (mkundu) kama kinyesi.

Muundo wa utumbo mpana

hariri

Urefu wake ni takriban mita 1.5 hivyo ni fupi kuliko utumbo mwembamba. Lakini ilhali ni nene zaidi huitwa "utumbo mpana". Umepangwa karibu kama duara inayoviringisha utumbo mwembana uliopo katikati.

Utumbo mwembamba unaunganishwa na utumbo mpana katika sehemu ya sikamu (ing. caecum). Upande wa chini ya sikamu kuna kibole (pia: kidole cha tumbo, ing. appendix)). Hii ni sehemu ya tumbo inayoweza kukabiliwa na ambukizo la hatari na tiba mara yningi ni upasuaji tu.

Kutoka hapa utumbo mpana unapanda juu hadi chini ya tumbo, baadaye unavuka nafasi ya tumbo kwa kulala, halafu unatelemka chini. Sehemu ya mwisho unapoelekea katikati ya mwili una umbo la "S" kwa hiyo huitwa utumbo wa sigma (ing. sigmoid colon).

Shemu ya mwisho ni puru au rektamu (rectum) na mkundu ambako mabaki ya chakula hutolewa kwa umbo la kinyesi.

Viungo vya Nje

hariri
  Makala hii kuhusu mambo ya anatomia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Utumbo mpana kama matumizi yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.