Uvuvi nchini Tanzania ni mojawapo ya sekta za uchumi nchini Tanzania. Sekta hii inachangia ukuaji wa uchumi wa Tanzania kwa kuuza samaki ndani na nje ya nchi hii, hivyo husaidia nchi kupata fedha za kigeni na kuboresha uchumi.

Shughuli ya uvuvi
Uvuvi nchini Tanzania

Maendeleo katika sekta hii si mazuri sana kutokana na ukosefu wa vifaa vya kisasa vinavyotakiwa kutumika katika uvuvi wa samaki, pia kutokufanya utafiti wa kutosha ili kuona na kujua maeneo yenye samaki wa kutosha. Hali hii inarudisha nyuma maendeleo ya uvuvi nchini.

Pia asilimia kubwa ya wavuvi Tanzania hawana elimu nzuri juu ya suala zima la uvuvi, hivyo huwapelekea kufanya uvuvi haramu: hii husababisha samaki na viumbehai wengine wa majini kupoteza uhai na hali hii inasababisha upungufu wa samaki katika bahari na maziwa yetu.

Inafaa kufuata njia bora za uvuvi ili kuboreha sekta hii ili kukuza uchumi bila kuharibu mazingira: katika baadhi ya mambo ni vizuri kuiga mfano wa nchi zilizoendelea katika shughuli za [uvuvi.

Serikali nchini inazidi kujitahidi katika kukuza sekta ya uvuvi kwa kuanzisha mbinu mbadala za ufugaji wa samaki, kwa mfano ufugaji wa samaki kwenye vizimba ziwa Viktoria, pia imezidi kutanua wigo kwa vijana kuweza kupata elimu ya ufugaji katika vyuo mbali mbali kwa kutambulisha vyema kozi zinazohusika na ufugaji wa samaki kama kozi ya AQUACULTURE inayopatikana katika vyuo vya SUA, UDSM na UDOM. Hali hiyo ni kutokana na samaki kuhitajika sana nchini kwa sababu ya ushauri wa wataalam wa afya kuwa ni chanzo kizuri cha protini. Pia ongezeko la watu kwa kasi limesababisha uhitaji wa nyama kuwa mkubwa ambapo samaki tu katika maziwa na bahari hawawezi kutosha kulisha taifa zima, hivyo ufugaji wa samaki kwenye vizimba na mabwawa Huhimizwa na serikali.

Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uvuvi nchini Tanzania kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.