Uwanja wa michezo wa Odi
Uwanja wa michezo wa Odi ni uwanja unaotumika kwa michezo mbalimbali huko Mabopane, Gauteng katika nchi ya Africa Kusini. Mara nyingi umekuwa ukitumika kwa mechi za mchezo wa mpira wa miguu. Uwanja huu una uwezo wa kuingiza watu wapatao 60,000. Ni uwanja wa nyumbani wa timu ya mpira wa miguu ya (Garankuwa United).
Uwanja wa ODI unapatikana Mabopane Kaskazini mwa Pretoria ndani ya mamlaka ya halmashauri yaTshwane Metropolitan.
Uwanja huo uliojengwa mwishoni mwa miaka ya 1980, unajivunia kuwa na vifaa vingi, ikiwepo viwanja vya mprira wa miguu, mchezo wa riatha, maonyesho ya kuruka juu, kurusha mkuki na nyundo n.k, seti nne za vyoo vya kiume na vya kike, chumba cha VIP na cha kupumzikia, chumba cha usalama, chumba cha waamuzi, Chumba cha udhibiti, Ofisi za usimamizi, Chumba cha jenereta, Stoo, Maeneo kadhaa kwa ajili ya michezo ya ndani, siti nne za juu pamoja na ofisi nne za tiketi.
Vituo vya nje ya eneo la uwanja inajumuisha nyumba ya [[klabu][, nyumba za wasimamizi, ofisi za mpira wa tenisi, mpira wa wavu pamoja na viwanja viwili visivyo rasmi vya mpira wa miguu.
Ubunifu wa uwanja huo unafanana na ule uwanja wa Mnabatho uliopo Mahikeng.[1]
Marejeos
hariri- Odi Stadium Archived 8 Juni 2021 at the Wayback Machine. at worldstadiums.com Archived 16 Machi 2006 at the Wayback Machine.
- ↑ Davis, Kitty (2019-03-26). What Happened to South African Stadiums After 2010 FIFA World Cup Archived 31 Oktoba 2023 at the Wayback Machine.. SA Stadiums. Retrieved 2020-04-09.