Valentina, Thea na Paulo
Valentina, Thea na Paulo (walifariki Kaisarea Baharini, leo nchini Israeli, 309) walikuwa Wakristo ambao waliuawa na gavana Firmiliano katika dhuluma ya kaisari Dioklesyano.
Hao mabikira wawili waliteswa kikatili wakachomwa moto baada ya Valentina kupiga mateke na kuangusha altare ya miungu, lakini Paulo alikatwa kichwa baada ya kupewa muda mfupi wa kusali na kuomba wote waokolewe [1]. Thea alitokea Gaza, Palestina.
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.
Tazama pia
haririTanbihi
haririMakala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |