Valery Twite Nahayo (amezaliwa mjini Bujumbura, 15 Aprili 1984) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka Burundi.

Valery Twite Nahayo
Maelezo binafsi
Jina kamili Valery Twite Nahayo
Tarehe ya kuzaliwa 15 Aprili 1984 (1984-04-15) (umri 40)
Mahala pa kuzaliwa    Bujumbura, Burundi
Urefu mita 1.90
Nafasi anayochezea Mlinzi
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa AA Gent
Namba 13
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
2008 Kaizer Chiefs
Timu ya taifa
2002 Burundi

* Magoli alioshinda

Kwa sasa anaichezea klabu ya Kaizer Chiefs katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini kama mlinzi. Ndiye kapteni wa timu ya Taifa ya Burundi.

Timu yake ya kwanza kabisa inaitwa Atomic F.C na Muzinga F.C mjini Bujumbura, baada ya hapo alipata fursa ya kujiunga na klabu ya Afrika Kusini ya Jomo Cosmos mwaka 2004. Mwaka 2008 aliweka saini katika klabu huko huko Afrika Kusini. Klabu hiyo ya Kaizer Chiefs ni mashuhuri sana huko Afrika Kusini na barani Afrika kwa ujumla.

Mechi yake ya kwanza kabisa kwa Kaizer Chiefs ilikuwa dhidi ya Manchester United tarehe 19 mwezi wa 7 mwaka 2008 na alionekana kuwa ni mchezaji mzuri kutokana na maneno aliyoyasema kocha wa Kaizer Muhsin Ertuğral, lakini alibadilishwa dakika 85 baada ya kujeruhiwa, na mechi hiyo ilikwisha sare 1:1.

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Valery Nahayo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.