Victoria Heilman

Msanifu wa majengo


Dkt. Victoria Heilman (alizaliwa 19 Februari 1973) ni msanifu majengo na mwalimu kutoka Tanzania. Yeye ana PhD katika Usanifu majengo kutoka Chuo Kikuu cha Stuttgart, Ujerumani shahada ya daraja ya pili ya Usanifu Majengo kutoka Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Amerika, Washington, DC na shahada ya kwanza ya Usanifu Majengo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Dkt. Heilman amechapisha makala nyingi za wasomi na ameshinda tuzo nyingi kwa kazi yake katika usanifu majengo.

Victoria Helman

Victoria Helman
Amezaliwa 19 Februari 1973
Bendera ya Tanzania Tanzania
Kazi yake msanifu majengo na mwalimu

Maisha

hariri

Dkt. Heilman alizaliwa katika Mkoa wa Mwanza nchi ya Tanzania. Katika mwaka wa 1996, alipokuwa na miaka ishirini na tatu alianza chuo kikuu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Anasema kwamba alifika katika usanifu majengo bila kujua ni nini. Yeye alisoma usanifu majengo katika Dar es Salaam kutoka 1996 hadi 2001. Katika mwaka wa 2004, Yeye aliondoka Tanzania kwenda kusoma Marekani. Amerika, Dkt. Heilman aliendelea kusoma usanifu majengo katika Chuo Kikuu cha Katoliki cha Amerika. Wakati akiwa Marekani, yeye alijitolea kwa Mazingira kwa Uanadamu. Baada ya yeye kupokea shahada ya daraja ipili yake, alirudi Tanzania na alijiunga upindi Utanzania ya Mazingira kwa Uanadumu. Wakati huu, Dkt. Heilman alifanya kazi kwenye mpango ya kijamii katika Zanzibar na Tanga.

Dkt. Heilman ni mmoja wa waanzilishi watatu wa Wasanifu wa Wanawake wa Kitanzania kwa Uanadamu (Tanzanian Women Architects for Humanity – TAWAH), chama cha wanasayansi wanawake na wasanifu majengo. Wanawake hawa wanaongoza katika ujenga nyumba katika jumuia zilizotengwa.

Yeye alifundisha katika Shule ya Usanifu Majengo na Usanifu wa Chuo Kikuu cha Ardhi. Dkt. Heilman anaishi nchi ya Tanzania. Hivi karibuni, yeye aliacha kufundisha, sasa yeye anajishughulisha na shughuli binafsi. Dkt. Heilman ni mmiliki wa VK Green Architects, kampuni ya usanifu majengo. Kampuni hiyo ilianzishwa mwaka wa 2011 na iko katika mji wa Dar es Salaam, nchi ya Tanzania. Wao wanasanifu na hujenga majengo ya kijani. Majengo ya kijani ni mazuri kwa mazingira na nguvu ya kufaa.

 
Leonard Mungarulire, Dkt. Victoria Marwa Heilman, na Salim Mohamed – Eisenhower Fellowships 2016

Machapisho

hariri
  • "Stakeholders Conceptualization of Sustainable Design and Construction in Tanzania." 9th Built Environment Conference Proceedings, ISBN 978-0-620-60356-0, 2015
  • "Education and Challenges of Female Architects in Tanzania" 4th Built Environment Conference Proceedings, ISBN 978-0- 620-43702-8, 2009
  • "Ten Years of Sustainable Construction, Perspective from a North Construction Manager and a South Architect's Point of View", SB08 Proceedings, ISBN 978-0-646-50372-1, Vol 3, Co - authored. 2008
  • "The Role of Research in Architecture" December 2007
  • "Helping Each Other Along the Way" July - Sept 2007, Ardhi University Official Newsletter, Vol 1. No. 1, ISSN 0856 -8553
  • "Gender and Architecture" May - August 2007 UDSM Gender Centre Newsletter, Volume 4 No. 2, ISSN 0856 - 972X
  • "Women in Architecture", April - June 2007 UCLAS Newsletter, ISSN 0856 8553
  • "Women in Architecture" titled "Education, Challenges and Architecture, The Case of Female Architects in Academia" 2007.

Marejeo

hariri
  Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Victoria Heilman kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.