Vijana jazz
Vijana Jazz (pia wanajulikana kama Vijana Jazz Band au Vijana Jazz Orchestra) ni bendi ya muziki wa dansi ya Kitanzania. Bendi hii ilipata umaarufu mkubwa katika miaka ya 1980. Vijana Jazz, kama bendi nyingine za dansi za nyakati hizo, ilifadhiliwa na taasisi ya serikali – Umoja wa Vijana. Umoja wa Vijana ulikuwa mrengo wa vijana wa chama tawala cha Tanzania – Tanganyika African National Union.[1] Wanamuziki mashuhuri ambao wamecheza katika Vijana Jazz ni pamoja na Hemedi Maneti, Issa Chikupele, na Manitu Musa.
Historia
haririBendi ilianzishwa mnamo mwaka 1971 na John Ondoro Chacha. Miaka miwili baada ya kuanzishwa, Vijana Jazz ilijiunga na mwimbaji na mtunzi wa nyimbo Hemedi Maneti.[2] ambaye alichukua jukumu kubwa katika kuongoza bendi hiyo na aliendelea kuongoza bendi hadi kifo chake mwaka 1990.[2] Walikuwa moja ya bendi ya kwanza kuchukua faida ya sheria iliyopitishwa na serikali ya Tanzania inayoruhusu bendi kununua vyombo vya muziki vya kigeni. Kabla ya sheria kupitishwa mnamo mwaka wa 1978, ununuzi wa vyombo vya muziki vya kigeni ulipigwa marufuku na Baraza la Muziki la Kitaifa - baraza la serikali linalohusika na kusimamia biashara ya muziki.[3] Vijana Jazz alichukua fursa hii na kuwa maarufu sana mwaka 1980 baada ya kuunda sauti mpya za ubunifu kwa kutumia synthesizers na ngoma za elektroniki.
Nchini Tanzania, bendi za muziki wa dansi zilianzisha mitindo mbalimbali ya muziki, maarufu kama mtindo. Mtindo wa Vijana Jazz ulikuwa maarufu kama "kamata sukuma", lakini pia walijulikana kwa mtindo wa "koka koka". Hata hivyo, mtindo wa Vijana Jazz pamoja na bendi nyingine za muziki wa dansi ulianza kupoteza umaarufu mwishoni mwa miaka ya 1980 wakati mfumo wa serikali ya Tanzania, Ujamaa, ulianza kushindwa. Uchumi wa nchi ulianza kudorora, na serikali ilishindwa kuwalipa wanamuziki tena..[3]
Vijana Jazz nchini Kenya
haririKatika miaka ya 1970, Kenya na Tanzania walikuwa washirika katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, na wanamuziki wa Kenya na Tanzania wangeweza kusafiri kwa uhuru kati ya nchi mbili kufanya kazi.[2] Muziki wa Tanzania ulikuwa maarufu nchini Kenya, na bendi za Kitanzania kama Vijana Jazz mara nyingi zilikuwa zikifanya ziara kutoka Dar es Salaam hadi Nairobi, ambapo zilikuwa zikicheza na kurekodi muziki.
Vijana Jazz walianza kurekodi muziki wao katika Polygram Records Kenya na A.I.T Records jijini Nairobi kwa sababu kama bendi zingine nyingi za muziki wa dansi zilikuwa na uhusiano mbaya na Radio Tanzania Dar es Salaam.[3] Katika miaka ya elfu moja mia tisa na sabini, Radio Tanzania Dar es Salaam ilikuwa studio pekee ya kurekodi nchini Tanzania. Bendi nyingi za muziki wa dansi zilisusia Radio Tanzania Dar es Salaam kwa sababu walijifunza rekodi zao ambazo zilikuwa za ujambazi na kutolewa Kenya. Bendi hizo hazikupokea malipo yoyote kwa rekodi zao. Pia, bendi hazikuwa na mipango ya mkataba, kwa hivyo wanamuziki hawakuweza kufuata mauzo ya muziki wao.[3]
Marejeo
hariri- ↑ Askew, K. M. (2002). Performing the Nation: Swahili Music and Cultural Politics in Tanzania. Chicago: University of Chicago Press.
- ↑ 2.0 2.1 2.2 Williams, S. (2011, December 18). Sex Batillion: The Koka Koka. Retrieved from African Business: https://african.business/2011/12/economy/sex-battalion-the-koka-koka/
- ↑ 3.0 3.1 3.2 3.3 Odidi, B. (2016, March 29). Tanzania as an East Africa musical powerhouse. Retrieved from Music in Africa: https://www.musicinafrica.net/magazine/tanzania-east-african-musical-powerhouse