Vincent wa Lerins (kwa Kilatini, Vincentius; alifariki 445 hivi) alikuwa mmonaki padri nchini Galia (leo Ufaransa), maarufu kwa maandishi yake ya teolojia na kwa juhudi zake za kufanya imani ya Wakristo istawi ndani mwao[1].

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa tarehe 24 Mei[2].

Maisha hariri

Vincent alizaliwa Toulouse. Baada ya kujitafutia maendeleo katika jamii, labda kama askari, aliamua kuingia monasteri ya Lérins kwenye kisiwa Saint-Honorat.

Akitumia jina bandia la Peregrinus aliandika huko Commonitorium (mwaka 434 hivi, yaani miaka 3 baada ya Mtaguso wa Efeso). Sawa na mtaguso mkuu huo, Vincent alitetea matumizi ya jina Mama wa Mungu kwa Bikira Maria, akipinga hoja za Nestori wa Konstantinopoli.

Eukeri wa Lyon alimsifu kama mtakatifu mwenye elimu na ufasaha mkubwa.

Gennadius wa Massilia aliandika Vincent alifariki chini ya makaisari Theodosius II na Valentinian III, kwa hiyo si baada ya mwaka 450. Masalia yake yanatunzwa huko Lérins.[3]

Commonitorium hariri

Lengo la Vincent katika kuandika Commonitorium[4] lilikuwa kubainisha vigezo vya kutofautisha ukweli wa imani Katoliki na uzushi, ili aweze kujikumbusha (ndiyo maana ya kichwa jicho).

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

Marejeo hariri

  • Thomas G. Guarino, Vincent of Lerins and the Devolopment of Doctrine. Grand Rapids: Baker Academic, 2013.

Viungo vya nje hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.