Virgil van Dijk alizaliwa 8 Julai 1991 ni mchezaji wa kulipwa kutoka nchini Uholanzi,ambaye anacheza kama beki wa kati katika klabu ya Liverpool na timu ya taifa ya Uholanzi. Anachukuliwa kuwa mmoja wa mabeki bora zaidi duniani, Van Dijk anajulikana kwa nguvu zake, uongozi na uwezo wake mkubwa katika mipira ya juu pindi awapo uwanjani.[1][2]

Virgil van Dijk
Virgil van Dijk

Baada ya kuanza ndoto yake ya mpira na klabu ya Groningen, Van Dijk alihamia Celtic mwaka wa 2013. Akiwa na Celtic alishinda Premiership ya Uskoti na alichaguliwa katika timu ya mwaka ya PFA ya Uskoti katika misimu yake yote miwili na klabu, na kushinda Kombe la Ligi ya Uskoti katika nafasi ya pili. Mnamo 2015, alijiunga na Southampton kabla ya kusajiliwa na Liverpool Januari 2018 kwa £75 million, ada ya uhamisho ya beki ambayo ilivunja rekodi ya dunia wakati huo.Akiwa na Liverpool, Van Dijk alicheza na kufikia fainali za UEFA katika 2018 na 2019, na kushinda.


Pia alitajwa kuwa Mchezaji bora wa mwaka wa Wachezaji wa PFA na mchezaji bora wa msimu wa ligi Kuu katika msimu wake wa kwanza. Van Dijk baadaye alishinda Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA la 2019 na UEFA Super Cup 2019, na kusaidia kumaliza ukame wa miaka 30 wa taji la ligi kwa kushinda ligi Kuu ya 2019-20. Ndiye beki pekee aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora wa kiume wa UEFA,na amemaliza wa pili kwenye kinyang'anyiro cha tuzo ya Ballon d'Or na mchezaji bora wa Wanaume wa FIFA, kwa mwaka huohuo wa 2019.[3]

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Virgil van Dijk kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. "Virgil van Dijk the best defender in the world, says Paul Merson". 
  2. "Virgil van Dijk: Champions League Defender of the Season", UEFA. 
  3. "The Best FIFA Men's Player". FIFA. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 7 Novemba 2016. Iliwekwa mnamo 2 Septemba 2019. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)"Virgil van Dijk wins UEFA Men's Player of the Year award", UEFA, 29 August 2019.