Visiwa vya Baleari

Ramani ya Baleari.

Visiwa vya Baleari (kwa Kikatalunya: Illes Balears) ni funguvisiwa vya bahari ya Kati, karibu na rasi ya Iberia, na ni sehemu ya Ufalme wa Hispania.

Visiwa vikubwa ni vinne: Majorca, Minorca, Ibiza na Formentera. Vingine ni vidogo.

Vile vikubwa vinapata watalii wengi wanaovutiwa na hali ya hewa na pwani.

Wakazi wamehesabiwa kuwa 1,106,049 (2010).

Lugha rasmi ni Kihispania na Kikatalunya.

Upande wa dini, wakazi wengi ni Wakristo wa Kanisa Katoliki.

Viungo vya njeEdit

  Balearic Islands travel guide kutoka Wikisafiri

Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Visiwa vya Baleari katika Open Directory Project