Vita ya miaka 100
Vita ya miaka 100 ilikuwa kipindi cha mapigano kati ya Ufaransa na Uingereza kilichodumu miaka 116 kuanzia mwaka 1337 hadi 1453.
Vita ilianza kwa sababu mfalme Charles IV wa Ufaransa aliaga dunia 1328 bila ya kumwacha mrithi, na mfalme Edward III wa Uingereza aliamini kwamba yeye mwenyewe ana haki ya kurithi cheo hiki kwa kuwa mama yake alitoka katika nasaba ya kifalme ya Kifaransa.
Wafaransa wengi walikataa na hii ilikuwa sababu ya vita.
Mwishowe Waingereza walipaswa kujiondoa katika Ufaransa mzima, hata katika maeneo makubwa waliowahi kuyatawala chini ya mamlaka ya jina tu ya mfalme wa Ufaransa.
Viungo vya Nje
hariri- England Hundred Years War Chronology World History Database Ilihifadhiwa 30 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- France Hundred Years War Chronology World History Database Ilihifadhiwa 30 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine.
- Timeline of the Hundred Years War Ilihifadhiwa 26 Machi 2017 kwenye Wayback Machine.
- Jean Froissart, "On The Hundred Years War (1337-1453)" Ilihifadhiwa 25 Desemba 2018 kwenye Wayback Machine. from the Internet Medieval Sourcebook
- The Hundred Years' War (1336-1565) by Dr. Lynn H. Nelson, University of Kansas Emeritus