Amon (kwa Kiebrania עַמּוֹן ʻAmmôn; kwa Kiarabu a=عمّون|t=ʻAmmūn), ni jina la kabila la zamani lililotawala upande wa mashariki wa mto Yordani, leo nchini Yordani.[1][2][3]

Mnara wa Waamoni huko Rujm Al-Malfouf, Amman, Yordani.
Qasr Al Abd ilijengwa na gavana wa Ammon kama mwaka 200 KK.

Mji muhimu zaidi wa Waamoni ulikuwa Rabbah au Rabbath Ammon, mahali pa Amman ya leo, makao makuu ya Jordan.

Waliabudu hasa Milkom na Molekh (pengine ni majina mawili ya mungu yuleyule).

Kwa mara ya mwisho uwepo wao unatajwa katika kitabu cha karne ya 2.

Tanbihi hariri

  1. Ancient Texts Relating to the Bible: Amman Citadel. University of Southern California. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-11-26. Iliwekwa mnamo 2011-01-11.
  2. MacDonald, Burton; Randall W. Younker (1999). Ancient Ammon. BRILL, 1. ISBN 9004107622, 9789004107625. 
  3. Levy, Tom; Øystein S. LaBianca and Randall W. Younker (1998). The archaeology of society in the Holy Land. Continuum International Publishing Group, 399. ISBN 0826469965, 9780826469960. 

Viungo vya nje hariri