Wabaski
Wabaski (kwa Kieuskara euskalduna) ni kabila la watu milioni 2-3 wanaoishi hasa Hispania kaskazini, lakini pia Ufaransa kusini-magharibi, mbali ya wengi waliohamia sehemu nyingine za dunia, hasa Amerika.
Lugha yao si kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya.
Kati ya Wabaski maarufu zaidi, kuna mapadri watakatifu Ignas wa Loyola na Fransisko Saveri, waanzilishi wa Shirika la Yesu, na Mikaeli Garicoits, mwanzilishi wa Mapadri na mabradha wa Betharram.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |