Wahamar
Wahamar ni jamii iliyoko kusini-magharibi mwa nchi ya Ethiopia. Wao wanaishi wilaya ya Hamer ambayo ni sehemu ambayo ina rutuba ya bonde la Mto Omo katika mkoa mwa Southern Nations, Nationalities, and People’s Region (SNNPR).[1] Idadi ya watu ambao wanaishi katika Hamar ni 60,000. Wahamar ni wafugaji na wana mila nyingi.[2]
Lugha ya Hamer-Banna
haririWahamar wanasema lugha ya Hamer-Banna ambayo ni lugha inayozungumzwa na makabila kadhaa nchini Ethiopia. Ni lugha mojawapo ndani ya lugha za tawi la Kiomotiki cha Kusini na za familia ya lugha ya Kiafroasia.[3]
Uislamu na dini za jadi
haririWahamar wanafuata dini mbili: Uislamu na Dini za jadi. Asilimia tisini na tano ya Wahamar ni Waislamu wa Sunni. Watu hawa wanaamini mafundisho matano ya msingi ya Uislamu.[4] Lakini, pia wanafuata sehemu nyingi za dini yao ya kitamaduni, Animisim . Wao wanaamini kuwa miti, miamba, wanyama, na vitu vingine vina roho. Na roho hizi ni muhimu sana kwa Wahamar.[5]
Nywele, Mavazi, na Mapambo
haririWanaume wanatengeneza nywele zao kwa udongo. Wanatumia rangi nyingi kama rangi nyekundu na nyeupe. Pia, wao wanavaa manyoya ya mbuni juu ya vichwa vyao kama mapambo. Wahamar wanavaa shanga za rangi nyingi na wanawake wanavaa vito vya chuma shingoni mwao. Mapambo ni muhimu sana kwa Wahamar.[4]
Ardhi ya Watu wa Hamar
haririKatika utamaduni wa Wahamar, ardhi haimilikiwi na mtu mmoja, lakini humilikiwa na wanajamii wote. Watu wote na wanyama wote wanaweza kulima na kufuga katika ardhi yoyote. Ng’ombe na ardhi ni muhimu sana kwa Wahamar.[6]
Wanaume na Wanawake
haririWanaume na wanawake wana majukumu tofauti katika utamaduni wa Wahamar. Wao wanafanya kazi tofauti. Kwa mfano, wanawake na wasichana hupanda mazao, huteka maji, hupika vyakula, na huwatunza watoto. Kwa upande mwingine, vijana hulinda wanyama na hupora wanyama kutoka kwa makabila mengine. Lakini, wanaume huchunga ng’ombe, hulima mashamba kwa kutumia ng’ombe, na hufuga mizinga ya nyuki. Ni kawaida kwa watu kufanya kazi kwa pamoja. Wanawake huwaalika majirani nyumbani kwao kusaidiana kazi kubwakubwa.[4]
Wazazi wanadhibiti watoto wao na kufanya maamuzi kuhusu ndoa zao. Kwa mfano, wazazi huwaambia wana wao lini watafunga ndoa. Wanaume wengi hufunga ndoa wakiwa na umri wa miaka thelathini. Lakini, wanawake huolewa wakiwa na umri wa miaka kumi na saba. Ndoa inahitaji mahari kutoka kwa familia ya bwana harusi kwenda kwa familia ya bibi harusi kama mbuzi, ng’ombe, na bunduki. Pia, Wahamar hawafungi ndoa na watu nje ya kabila lao.[4]
Familia nyingi zinadhibitiwa na wanawake kwa sababu wanawake wanaishi muda mrefu kuliko wanaume mara nyingi. Mjane hudhitibiti ndugu wadogo na ng’ombe wa mume wake baada ya kifo cha mume wake.
Mila za Kuruka Fahali
haririWahamar wana mila za kuruka fahali.[6] Desturi hii inaingiza mwanaume katika uanaume. Kabla ya kufanyiwa jando kwa mvulana, nywele za mvulana hunyolewa. Halafu, yeye anapakwa mchanga ili kuosha dhambi na kupakwa kinyeshi ili kupata nguvu. Pia, anavaa gome katika umbo la msalaba ili kulinda roho yake. Wavulana wanahitaji kukimbia juu ya migongo ya mafahali mara mbili. Kama mvulana anaanguka, yeye anadhihakiwa. Kama mvulana anafanikiwa kukimbia juu ya migongo ya mafahali mara mbili, anaarikiwa na kutakuwa na ngoma kubwa. Wakati wa kuruka ng'ombe, jamaa ambao ni wasichana wanacheza na wanataka kuchapwa viboko na wanaume. Kuchapwa viboko kunaonyesha msaada wao kwa mtu ambaye amefanyiwa jando. Kuchapwa viboko husababisha deni kati kijana na dada yake. Mokovu mgongoni mwake yanaonyesha kumuunga mkono kaka yake. Kwa sababu hii, mwanaume atahitaji kumsaidia dada yake katika siku zijazo. Desturi hii inaruhusu mwanaume kuoa, kumiliki ng’ombe, na kupata watoto.[6]
‘Mingi’
haririKuna desturi ambayo inaitwa ‘mingi’ katika utamaduni Wahamar. Wanawake ambao hawajaolewa wana watoto ili kupima uwezo wao wa kuzaa. Lakini watoto wengine huwekwa porini na kuachwa wafe. Hii ni kwa sababu Wahamar wanaamini kuwa watoto ambao kuzaliwa nje ya ndoa wana ‘mingi’ ambayo ni laana ya shetani. Mingi husababisha majanga kama ukame na magonjwa. Kwa hivyo, mtoto anauawa.[4]
Desturi ya Kahawa
haririKahawa hupandwa katika ardhi ya Wahamar. Ni desturi kwa wazee na wakuu kunywa kahawa na mtu kabla ya kusafiri. Mzee atasema baraka na kisha kumtemea mtu kahawa iliyojaa mdomoni. Katika utamaduni Wahamar, hii itambariki mtu huyo.[1]
Wakati Ujao
haririBarabara na miji inapanuka katika sehemu hii ya Bonde la Omo. Watu wengi wamehuria mjini, wamekwenda shuleni, na wamebadilisha desturi.[6]
Marejeo
hariri- ↑ 1.0 1.1 Excelman Productions. "The Hamer People ( Hamar tribe ) of the Omo Valley : Bull Jumping - Excelman Productions | Filming in Ethiopia : photos of a Field Producer". The Hamar People of the Omo Valley : bull jumping - Filming in Ethiopia : Excelman Productions | Television Production Services, Field Producer, Line Producer (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-04-08.
- ↑ "Hamar people", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-12-25, iliwekwa mnamo 2023-04-08
- ↑ "Hamer language", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2021-10-10, iliwekwa mnamo 2023-04-08
- ↑ 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 atlasofhumanity.com. "Ethiopia, Hamer Tribe". Atlas Of Humanity (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-04-08.
- ↑ "Hamar people", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-12-25, iliwekwa mnamo 2023-04-09
- ↑ 6.0 6.1 6.2 6.3 "BBC - Tribe - Hamar". www.bbc.co.uk. Iliwekwa mnamo 2023-04-08.