Wakisii (hujulikana pia kama Abagusii au Gusii) ni kabila la Kibantu ambao hukaa katika kaunti ya Kisii na kaunti ya Nyamira, magharibi mwa Kenya.

Kisii - mji unaojulikana na wakazi wake kama Bosongo au Getembe - uko kusini magharibi mwa Kenya na ni nyumbani kwa watu wa asili ya Gusii. Jina Bosongo liliaminiwa kutokana na jina Abasongo (kwa maana ya Wazungu) ambao waliishi katika mji wakati wa ukoloni.

Mwaka 2014 walikadiriwa kuwa 3,205,669.

Asili ya Abagusii

hariri

Waabagusii pamoja na makundi mengine ya Kibantu wanaaminika kuwa na asili ya Zambia. Kuhama kwao kunaaminika kuwa kulitokana na wakazi zaidi, uhaba wa chakula, migogoro kati yao na udongo uliopotewa na uzuri wake kwa ajili ya kilimo. Wabantu walipokuwa wakitoka Kongo, waligawanyika katika makundi mbalimbali na Wakisii waliishia kuishi karibu na Ziwa Viktoria.

Kuna wengine walibaki Songea na sasa hujiita Wakisi ila jina kamili ni Wakisii. Wanapenda ufugaji na kilimo. Hupenda kuishi maeneo ya wazi. Katika safari ya kutoka Zambia Walipita Songea, kiasi fulani wakabaki na wengine walibaki Mkoa wa Mara waliosalia wakaenda hadi Kenya

Wakisii waliishia katika eneo la kijiografia la kipekee miongoni mwa makundi ya Kibantu kwani walikuwa wamezungukwa pande zote na makundi ya maadui ya Kinailoti ya Wajaluo, Kipsigis, Wanandi na Wamaasai. Ubishani usioisha uliwafanya wawe na desturi ya vita ili wajihami dhidi ya wezi wa mifugo. Hadi siku hii, wana sifa ya kuwa wagumu, wasiopoteza roho haraka, na wanaofanya kazi sana.

Wakisii leo

hariri

Wakisi wanajulikana kama mojawapo ya jamii zinazojishughulisha zaidi Kenya, waliobarikiwa na mashamba makubwa ya chai, kahawa na migomba. Hata hivyo, kaunti ya Kisii ina msongamano mkubwa sana wa watu. Ni moja ya maeneo yaliyo na watu wengi sana nchini Kenya (baada ya miji ya Nairobi na Mombasa), na yenye watu wengi zaidi katika maeneo ya mashambani.

Pia ina moja ya idadi kubwa zaidi ya uzalishaji nchini Kenya (kama inavyothibitishwa na mfululizo wa demografia na utafiti). Idadi ya uzalishaji katika jamii ya Wakisii ni mojawapo ya za juu zaidi ulimwenguni [1]. Mambo haya yamefanya Wakisii kuwa miongoni mwa jamii zilizoenea zaidi kijiografia katika Afrika Mashariki.

Idadi kubwa ya Wakisii pia imekwenda ugenini kutafuta masomo ma maisha mazuri zaidi. Wakisii ni baadhi ya Wakenya wengi zaidi kuwakilishwa katika vyuo vikuu vya kigeni (kawaida India na Marekani).

Majina kama Mogeni, Bogonko, Osebe, Bosire, Moseti, Onkoba, Onchiri, Isaboke, Kiberi, Mogaka na wengine ni majina ya familia ya kawaida tu kama Smith na Johnson katika tamaduni za Anglo-Saxon. Majina ya kike kama Moraa, Nyanchama, Nyaboke, Kemunto, Kwamboka, Kerebi na mengine pia ya kawaida yaliyotolewa kwa wasichana.

Kilimo

hariri

Kitambo kilichopita, Kisii ilikuwa na misitu mikubwa, pamoja na miti iliyozeekana yenye matawi pana. Ilikuwa ni sehemu ya msitu wa Bonde la Kongo. Mabaki ya pekee ya msitu huu Kenya ni msitu Kakamega, ambao ni pembe magharibi zaidi ya msitu wa Ikweta. Maeneo mawili ya misitu huo yalikuwa yanaunganishwa kupitia Nandi na Kericho, kabla ya maeneo ya Nandi na Kericho kukatwa miti ili chai ipandwe na matu wakae pale.

Wao wanazungumza lugha ya Kisii au Ekegusii kama inavyojulikana miongoni mwa wasemaji. Hata hivyo, baadhi ya makala ya kitambo huita jamii hii Kosova. Lugha hii na lugha nyingine za Kibantu ni sawa sana. Wameru wanafanana sana na Wakisii katika lugha na utamaduni. Pia Wakisii na Wakuria lugha zao zinafanana sana: inadhihirika asilimia 79 ya maneno hufanana.

Utamaduni

hariri

Wakisii hucheza kiungo kikubwa cha muziki kiitwacho obokano.

Tohara ni mojawapo ya sherehe ambapo vijana walijifunza jinsi ya kuishi na kuheshimu wakuu wao. Vijana ambao walikuwa wanatahiriwa walifunzwa jinsi ya kujitahidi katika kutafutia jamii yao. Kutahiri kwa vijana wenye umri wa miaka 10 kunafanyika bila dawa za kupunguza uchungu.

Wakisii mashuhuri

hariri

Viungo vya nje

hariri
  Makala hii kuhusu utamaduni wa Kenya bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakisii kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. Kenya Conundrum: A Regional Analysis of Population Growth and Primary Education (Paperback) by 'Juha I. Uitto [Mwandishi]