Wanawake wa Angola
Wanawake wa Angola, kama wanawake wengine wa Afrika, wana majukumu mbalimbali katika jamii ya nchi ya Angola.
Majukumu yao
haririHakukuwa na utafiti kuhusu majukumu ya wanawake wa Angola kufikia miaka ya 1980, lakini kulikuwa na vipengele vya kijumla ambavyo vingeweza kuafikiwa kuwahusu.
Ukulima
haririKatika maeneo ya vijijini ya Angola, idadi kubwa ya watu walijihusisha na ukulima. Wanawake walifanya nyingi kati ya kazi ya ukulima.
Ndoa
haririKwa ujumla, ndoa ilijumuisha utilizi maanani wa familia, siasa na masuala ya uchumi na vilevile mahitaji ya binafsi. Jamii ilipewa kipaumbele katika ndoa. Jamii ya nyumbani ndiyo ilikuwa msingi wa uzao na ilishirikisha marika mbalimbali.
Wanawake walikuza na kutayarisha chakula cha familia mara nyingi, na kufanya kazi nyingine za nyumbani. Kwa sababu ya majukumu yao mengi, wanawake walikuwa na hati karibu sawa na wanaume, ambao waliupitisha muda wao mwingi katika kuwinda na kulisha ng’ombe.
Chama cha Wanawake cha Angola
haririWanawake wengi walijiunga na Chama cha Wanawake cha Angola (Organização da Mulher Angolana - OMA). Kabla ya uhuru, OMA kilikuwa chombo muhimu katika harakati za kuwahamasisha wakimbizi wengi wa Angola kukiunga mkono chama cha MPLA kilichopigania uhuru.
Baada ya uhuru, hasa baada ya kuundwa kwa MPLA-PT mnamo 1977, vyama vyote viliwekwa chini ya utawala mkali wa chama hicho na vilipewa jukumu la waunganishi kati ya MPLA-PT na wananchi.
Mnamo 1987, OMA ilikuwa na uanachama wa takribani milioni 1.3, wengi wao wakiishi sehemu za mashambani za nchi.
Michango ya OMA
haririKati ya michango mingi ya OMA ilikuwa uanzishaji wa miradi ya elimu kwa watu wazima na pia mashirika ya kutoa huduma za kijamii.
Changamoto za shirika la OMA
haririWengi wa wanachama, hata hivyo, hawakuwa na ajira na walikuwa maskini. Kufikia mwaka 1988, asilimia 10 pekee ya wanachama wa MPLA-PT walikuwa wanawake, ingawa wanawake wengi walianza kupata ajira katika ualimu na kazi nyingine walizokuwa wametengwa nazo awali.