Wandamba ni kabila la Tanzania wanaoishi kiasili katika mkoa wa Morogoro, Wilaya ya Malinyi na Wilaya ya Kilombero, hasa katika mji wa Ifakara pamoja na vijiji vya Mofu, Ruipa, Mbingu, Mngeta, Merera, Chita, Ngombo, Mlimba na Biro. Wa wanapatikana pia katika wilaya ya Ulanga katika kijiji cha Malinyi.

Lugha yao ni Kindamba (wenyewe wanatamka Chindamba), ambacho kinafanana sana na Kimbunga (69%) na Kipogoro (56%), lugha ya Wapogoro wanaoishi katika wilaya ya Ulanga. Hiyo inathibitisha kwamba asili yao ni moja.

Upande wa dini wengi wao ni wafuasi wa Yesu Kristo katika Kanisa Katoliki.

Mwaka 1987 walikadiriwa kuwa 79,000, mbali ya Wambunga waliokuwa 29,000.

Ni maarufu kwa kupenda kula wali na samaki hata mwaka mzima.

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wandamba kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.