Upelaji
(Elekezwa kutoka Wapelaji)
Upelaji (kwa Kiingereza: Pelagianism) ni mtazamo wa teolojia ya Ukristo unaodhani dhambi ya asili haijaharibu umbile la binadamu, hivyo hiari yake inaweza bado kutekeleza maadili bila kuhitaji neema ya pekee kutoka kwa Mungu. Hatimaye mtu anaweza kujipatia wokovu kwa juhudi zake mwenyewe.

Mtazamo huo umepata jina kutokana na mmonaki wa Ireland[1] Pelagius (354–420 au 440), ingawa pengine huyo alikataa baadhi ya mafundisho yaliyosemekana kuwa yake.
Ulipingwa hasa na Agostino wa Hippo na kulaaniwa na mtaguso wa Kartago wa mwaka 418, halafu na mtaguso wa Efeso (431).
Hata hivyo unajitokeza tena na tena katika historia ya Kanisa, hasa katika makundi yenye juhudi katika maisha ya Kiroho kama upelajiupande.
Tanbihi hariri
- ↑ (1901) "Pelagius in Ireland", 20.
Vyanzo hariri
- Bercot, David. A Dictionary of Early Christian Beliefs, Hendrickson Publishers
- Rees, B. R., The Letters of Pelagius and his Followers, The Boydell Press
Marejeo mengine hariri
- Maandishi ya Pelagius
Viungo vya nje hariri
- The Writings of the legendary Pelagians Archived 6 Januari 2017 at the Wayback Machine.
- Canons From The Council Of Carthage Against Pelagianism, May 1, 418
- Pelagians, Donatists, Monks, Anabaptists and other Perfectionists Archived 11 Februari 2006 at the Wayback Machine. – a sympathetic look at Pelagianism and similar 'perfectionist' movements
- Pelagius Library Archived 1 Machi 2021 at the Wayback Machine.: Online site dedicated to the study of Pelagius
- Pelagianism: The Religion of Natural Man Archived 1 Aprili 2007 at the Wayback Machine. – a critical look at Pelagianism
- Marcus, Gilbert. "Pelagianism and the ‘Common Celtic Church’", University of Glasgow
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Upelaji kama historia yake, matokeo au athari zake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |