Wapiga Ngoma wa Kifalme wa Burundi
Wapiga Ngoma wa Kifalme wa Burundi (The Royal Drummers of Burundi) ni kundi la ngoma kutoka Burundi, moja kati ya vikundi vikubwa vya ngoma duniani. Mtindo wa upigaji ngoma wa kikundi unaitwa Inkiranya.
Historia
haririKatika Burundi ya zamani, ngoma zilikuwa zaidi ya ala rahisi. Ngoma zilikuwa vitu vitakatifu na zilitumia kwa matambiko. Wapiga ngoma walitumbuiza kwenye kutawazwa wafalme, mazishi, na matukio mengine muhimu. Wapiga Ngoma wa Kifalme wa Burundi hapo awali waliandamana na Mwami katika safari zake.
Muziki wa Wapiga Ngoma
haririWapiga Ngoma wa Kifalme wa Burundi wanapiga ngoma kwa shauku na kucheza muziki, kuruka, na kuimba. Mwanzoni mwa tukio, wanaume thelathini huingia na ngoma juu ya vichwa vyao na kuunda nusu-duara.[1] Wanaume huvaa mavazi ya kitamaduni ya rangi nyekundu, kijani, na nyeupe. Wapiga ngoma wanaruka na wanazunguka kwenye ngoma kubwa ya katikati. Ngoma kubwa inaitwa “karyenda.”[2] Pia, ngoma ya "amashako" inatoa mdundo unaoendelea. Ngoma za “ibishikiso” hufuata mdundo wa ngoma ya kati ya “inkiranya.” Mipigo ya msalaba inawakilisha nyakati ngumu na mafadhaiko ya kijami ambayo watu wanayo, na mapigo makuu huwakilisha kusudi la maisha wakati wa kukabiliana na changamoto za maisha. Waafrika wanasema kuwa midundo hiyo inawakilisha maisha na kutegemeana katika mahusiano ya wanadamu. Gabriel Ngatabo, mkurugenzi wa Wapiga Ngoma wa Kifalme wa Burundi, alisema kuwa “Mawasiliano kwa njia ya ngoma yanaelezea kile kinachotokea katika Mtazamu wa Kiburundi.”[3]
Ngoma
haririNgoma zinazotumiwa na Wapiga Ngoma wa Kifalme wa Burundi sio ngoma za kawaida. Ngoma hizo zimetengenezwa kutoka kwa shina la mti uitwao "D’umuvugangoma" likimaanisha "mti unaofanya ngoma zizungumze." Wapiga ngoma hupanda mbegu za miti ili kutengeneza ngoma zaidi kwa ajili ya vizazi vijavyo. Ngoma ni chombo muhimu na, kama ilivyo kwa mwanamke, inaonekana kama kitovu cha maisha, kwa hivyo, ngoma inawakilisha umbo la mwanamke. Uhusiano kati ya ngoma na asili ni nguvu sana pia. Kwa hivyo, sehemu tofauti za ngoma zimepewa jina la dhana ya uzazi:
- Ichai ni ngozi ya ngoma na inawakilisha ngozi ya mama.
- Amabere ni vigingi vya ngoma na inawakilisha matiti ya mama.
- Urogori ni kamba inayonyoosha ngozi ya ngoma na inawakilisha taji ya uzazi
- Inda ni silinda ya ngoma na inawakilisha tumbo la mama.
- Umukondo ni mguu wa ngoma na inawakilisha kitovu[4]
Nje ya Burundi
haririTangu mwaka 1960, Wapiga Ngoma wa Kifalme wa Burundi wamezuru nje ya nchi ya Burundi. Sasa, wanacheza kwenye kumbi za tamasha maarufu na sherehe kote ulimwenguni. Wanamuziki wa Magharibi walipenda “beti ya Burundi” kama wanamuziki kama Joni Mitchell, Adam and the Ants, na Bow Wow Wow. Wapiga Ngoma wa Kifalme wa Burundi wanaonekana kwenye albamu ya Joni Mitchell, The Hissing of Summer Lawns (1975).[2] Pia, kikundi kilimtia moyo Thomas Brooman kuunda tamasha la WOMAD katika mwaka elfu moja mia tisa tisini na mbili (1982). Wamerekodi albamu tatu.
Sasa
haririSasa, ngoma bado ni muhimu katika nchi ya Burundi. Wapiga Ngoma wa Kifalme wa Burundi wanacheza ngoma kwenye sherehe za kienyeji na hafla za kitaifa. Watu wa Burundi wanafikiri kuwa Wapiga Ngoma wa Kifalme wa Burundi ndio wawakilishi muhimu zaidi wa nchi wa tamaduni za muziki za Burundi. Wao wameliweka kundi hai kwa miaka mingi na wameshiriki upigaji wao wa ngoma na watu wengine ulimwenguni.[3]
Marejeo
hariri- ↑ "THE ROYAL DRUMMERS OF BURUNDI: DRUMMERS OF PEACE AND ONE OF THE WORLD`S GREATEST PERCUSSION ESEMBLES". THE ROYAL DRUMMERS OF BURUNDI. Iliwekwa mnamo 2022-04-19.
- ↑ 2.0 2.1 "Drummers of Burundi - World Music". www.worldmusic.co.uk. Iliwekwa mnamo 2022-04-19.
- ↑ 3.0 3.1 Dr Cheryl Paulhus (2012-10-07). "'The Royal Drummers and Dancers of Burundi' at George Mason University by Dr. Cheryl Paulhus". DC Metro Theater Arts (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-25. Iliwekwa mnamo 2022-04-19.
- ↑ "Sacred rituals of drummers and dancers of Burundi". Village Life. 2012-11-08. Iliwekwa mnamo 2022-04-19.