Wikipedia:Kuheshimiana

(Elekezwa kutoka Wikipedia:Civility)

Kuheshimiana ni shabaha na msingi wakati washiriki wa wikipedia wanawasiliana.

Wakati mwingine tunaweza kutofautiana kuhusu habari zinazojadiliwa katika makala. Hata tukijaribu kutosimama upande mmoja kama tunatambua kuna maoni tofauti kuhusu jambo, mhariri mwingine anaweza kufikiri ya kwamba makala inakosa habari muhimu au kuelekea upande.

Hapa ni muhimu tuheshimiane kati yetu. Sisi sote ni watu wanaojitolea bila malipo. Sisi sote tunashiriki kujenga kamusi elezo ya kwanza kwa lugha ya Kiswahili.

  1. Tusipoteze muda kuvutana na kugombana kwa hasira.
  2. Badala yake tusaidiane na kushauriana,
  3. Tuepukane na maneno makali kama tunatofautiana kuhusu makala.
  4. Tutafute ushauri wa washiriki na waratibu wengine kama tunashindwa kuelewana na mwenzetu.