Wikipedia:Kiswahili Wikipedia Challenge/Submissions/Kiswahili Wikipedia Challenge/Submissions

KWC Mtumiaji huyu ni mwanafunzi katika JKUAT.
KWC Mtumiaji huyu ni mshiriki katika Shindano la Wikipedia ya Kiswahili la 2009.   (Submissions)


|- | KUISHI NA TUMAINI NA UPENDO KWA NCHI YANGU || worked by Abdallah Aboud. translated from en. KUISHI NA TUMAINI NA UPENDO KWA NCHI YANGU By Cecilia Pereruan Naeku Egerton University Kukuzwa katika tambarare ya Narok ilikua hisia nzuri. Masahibu zangu na huwa napenda kuchukua njia ndefu kutoka shule na kutumia muda huu kwa ujunja tulonao kuzunguka njia za msituni, kucheza, kufukuzana mmoja kwa mwingine na mara chache kukusanya matunda ya mwituni - sananguru. Na wakati tukifika nyumbani ilikuwa inakaribia jua kukutwa na ng'ombe wameregea kitambo kutoka malishoni. Wakati mwingine tulichapwa makalioni (kwa sasa ni jambo lililokua tumeanza kulizoea), au bahati hutulemea upande wetu na tulitoroka. Lakini kumbukumbu zangu wazi zaidi ni watu wa ajabu na wakuvutia kutoka nchi zilizo kando na bahari (tunaweza wahukumu kwa rangi ya ngozi zao) ambao hutumia barabara yetu yenye vumbi wakielekea Mara. Hukimbia kuelekea barabarani haraka mara tunapoliona vumbi kutoka kwa gari likikaribia kwambali. Hukukimbia kwa hamu kiasi kwamba hupuuzilia miiba inayotudunga miguuni mwetu (huhisi maumivu baadaye). Tuliwaangalia kwa mda, tumepigwa na bumbuwazi, vinywa viwazi, ni mfano wa tuloona viumbe vya ajabu kutoka ulimwengu wa “Mars”. Ni jambo la kufurahisha kwa sababu watalii kuja kuona wanyama wa pori lakini waliiishia kuwa kivutio kwetu pia.

Miaka kumi na tano baadaye na idadi ya wageni wanaomiminika ndani ya nchi yetu kuona na kushuhudilia wanyama wa pori na kupumzika katika maangazio mazuri ni jambo bado la nishangaza.Kenya, nchi yangu ni nchi ya maajabu, yenye urembo ulokamilika.

Kumbukumbu hizi zinazonijia kama majuto nikijaribu kupata uwiano kati ya mambo ambayo wakati mwingine hunifanya nigeuze kichwa changu kwa aibu na mara nyingine kukiinua - yote juu ya kuwa Kenya. Ndiyo, ni kweli kwamba Kenya inasumbuliwa na ugonjwa huu wa ulemavu wa rushwa. Ndiyo, ni kweli kwamba wengi wa wananchi wetu wanaishi chini ya mstari wa umaskini, na ni kweli kwamba tuna uhaba mkubwa wa kilakitu pande zote. Lakini lazima changamoto hizi kutufanya kupoteza imani ndani yetu? Lazima wao kutufanya kuachana na matumaini na kukumbatia tamaa?

Mama yangu daima huniambia kuwa Mungu Hafanyi makosa. Kuna azma ambayo Mungu alituweka hapa kuwa Wakenya. Kulingana na mimi, azma, ambayo ni rahisi kusema kuliko kufanywa - na mimi daima natafuta ujasiri wa kuishi ili kuifanikisha- ni kuiacha nchi hii kwa ubora kuliko nilivyo ipata. Sijui unavyofikiria na jinsi unavyohisi,lakini nimeshawishika kwamba sisi sote kuna sababu kuwa ndani ya Kenya, sio Amerika, siyo Somalia, lakini Kenya.

Kujivunia kuwa mkenya inaweza kuwa suluhisho kwa baadhi ya matatizo yanayotukabili sasa. Askari polisi mwenye heshima ya juu katika kazi ya kulinda raia na ni fahari kwake kutumikia nchi yake hatojiingiza katika kula hongo na rushwa kwa sababu mienendo haya huchafua sifa ya nchi yake. Yeye kuwa na ufahari wa kuwa mkenya hangekua na moja kati ya haya. Madaktari bora wa Kenya, kukuzwa na kufunzwa Kenya au pahali pengine, wangechagua kufanya mazoezi nchini Kenya,ijapokua kuna vikwazo vya fedha, kama kweli walikuwa wanajivunia kuwa wa Kenya. Wanasheria bora wangekuwa wanachagua kubakia na kuwasaidia watu wao badala ya kuwashughulikia wageni matajiri pahali pengine.

KamaTungejichukulia majivuno wenyewe, tungechagua kuwapa watoto wetu elimu bora kuwaokoa kutoka katika umaskini ambao ni kama ugonjwa ulokomaa. Watoto wetu wlojihami na elimu bora wangekuwa na nafasi nzuri katika siku za usoni. KamaTungejichukulia majivuno wenyewe katika ardhi yetu, tungechagua kuhifadhi mazingira ya viumbe, misitu na wanyamapori wetu. Sisi wote kikamilifu tunafahamu kwamba utalii inachangia pakubwa katika kuleta pesa za kigeni nchini mwetu.Yalitokea wapi haya mahimizo ya kijuha kuwa tuharibu misitu yetu yote? Kwa nini tujizamishe ndani katika hili shimo la umaskini? Kwa nini tujichimbie makaburi wenyewe? Maarifa ni nguvu. Ni mantiki ya urahisi kwamba ukataji wa miti na kuharibu misitu itapunguza kiwango cha mvua. Kupungua kiwango cha mvua husababisha ukame, na ukame hutafsiriwa kama kifo. Hivyo Wakenya walonaufahari, tuokoe mazingira ya viumbe, hebu tujiokoe wenyewe na vizazi vitakavyo kuja baada ya sisi.

Pengine njia ya uhakika ni kuishi kwa ujasiri na kwa kueleweka,ni kutumikia wengine. Dini zijulikanazo nchini Kenya, nazo ni Ukristo, Uislamu, dini ya jadi ya Afrika na ‘Hinduism’, yote yanasisitiza haja ya kufanya mazuri kwa binadamu. Tunapaswa kujifunza kuishi vizuri na majirani wetu licha ya tofauti kati yetu. Mchafuko wa ghasia za uchaguzi wa 2007 ulileta aibu sana kwetu huku dunia nzima ikitutazama tukiwakataka wananchi wenzetu, bila ya huruma tukiwanyima makaazi yao na kukatisha matumaini yao. Hili lilikuwa jambo kubwa la kuturejesha nyuma na kutuweka katika hali ya kutisha. Ingawa kurejeshwa nyuma ni kuanzishwa kwa kurejea. Ndio sababu naendelea kuwa na matumaini. Na hivyo lazima sisi wote kama Wakenya. Nina matumaini katika kujenga jina letu na sifa zetu.

Kenya nzuri haitokei tu, ni sisi kuifanya itokee. Ili kupata ufahari kutokamana na kitu, nikufanya kitu ambacho tutajivunia nacho. kupitishiana lawama na kulalamika inawezakana kuwa asili ya binadamu lakini pia ni kuangamia kwetu. Badala ya kulaumu changamoto nyingi zitukumbazo, hebu tufanyeni kitu, chochote,katika hali yoyote tutakayo kuwa. Hebutuwe na majivuno ya nchi yetu na kufanya kitu cha kusifika iwe nzuri. Tunahitaji kuwa na dira kwa nchi yetu; ukosefu wa maono ni kifo chetu.

Kusukumwa kuwa mkenya kwa ajili yangu ni kwa haya yote tulioyataja juu. Kuifanya Kenya ni bora kutumia hali yangu kama mwanafunzi, kusoma kwa bidii na kuitumikia nchi yangu. Kuhifadhi mazingira kwa njia yoyote niwezavyo, kujifunza vipi kuishi na kwa majirani zangu.

Licha ya mawingu kwamba wakati mwingine kukusanyika na wasiwasi mara kwa mara hutokea, najua siwezi kumudu kupoteza matumaini. Sisi kama Wakenya hatuwezi kupoteza matumaini ndani yetu. Tunapaswa kuwa na imani na sisi wenyewe na kuangalia mbele kwa mustakabali wa kufanya nchi hii bora.

Fikiria wa baba zetu ambao walipigana kwa uhuru wetu kwa damu yao, siyo kujali kuhusu maisha yao lakini juu ya uhuru wetu. Walitufikiria sisi katika mapambano ya kupigania uhuru. Je, walijitahidi bila ya mafanikio? Ilikua kupigania uhuru kwao sichochote? Hakika sivyo. Kama hatuwezi kuchukua majivuno sisi wenyewe, hakuna katu atakaye tufanyia.

[[1]]