Wikipedia:Kuzuia watumiaji

Watumiaji wanaweza kuzuiwa kama wanasababisha uharabu kwenye kurasa zetu. Azimio la kumzuia mtumiaji linachukuliwa na mkabidhi.

Mara nyingi tutamzuia mtumiaji "milele" kwanza, ilhali tunampa nafasi ya kuwasiliana na mkabidhi (kupitia "email this user") na kuonyesha hakuwa na nia mbaya. Halafu tutamrudisha kwa siku 1-3 hivi na wakati huo ana nafasi ya kusahihisha makosa yake. Baadaye wakabidhi tukague kama amesahihisha. Kama amemaliza kusahihisha kiasi cha kuonyesha nia njema na uwezo, tumfungue kabisa. Kama bado, siku 3 tena hadi tunaridhika. Au abaki nje.

Sababu kuu za kumzuia mchangiaji ni pamoja na

Makosa mazito

  1. kuondoa hovyo yaliyomo kwenye ukurasa, kuingiza matusi au matini ambayo ni dhahiri haina maana.
  2. kuingiza matangazo wa biashara, hasa kwa siri, yaani kwa kuficha tabia yake ya kweli.
Watumiaji hao wasirudishwe.

Kuingiza tafsiri ya kompyuta bila sahihisho ya kutosha

    1. Kama mchangiaji amewekewa sanduku la “Karibu” (99%) ameshaona ni mwiko kumwaga matini ya tafsiri ya kompyuta. Kwa hiyo, kama anapakia matini ambayo ni tafsiri ya kompyuta yenye makosa atazuiwa halafu tuweke alama za Kigezo:Zuia tafsiri kwenye ukurasa wake wa majadiliano. Ni alama hizo: {{Zuia tafsiri}} ~~~~. Kabla ya alama ya sahihi ~~~~ tunaweza kuongeza sababu za ziada.
    2. Kila mkabidhi anayetumia njia hii anapaswa kuwezesha nafasi ya “Email this user”. Vinginevyo tufuate maelezo kwenye Kigezo:Zuia tafsiri (https://sw.wikipedia.org/wiki/Kigezo:Zuia_tafsiri). Anaweza kukubaliwa tena katika utaratibu uliotajwa juu.

(Utaratibu umekubaliwa na wakabidhi kupitia Majadiliano_ya_Wikipedia:Wakabidhi#Utaratibu_wa_kuzuia_wanaoleta_tafsiri_ya_kompyuta_na_kuandaa_editathon_ya_kutafsiri_makala (Agosti 2021) na kwenye kundi la Telegram la wakabidhi tarehe 25 Novemba 2021.

Tazama pia

Maalum:OrodhayaIPZilizozuiliwa