Wikipedia:Makala kwa ufutaji/Nyaraka 4

Hii ni nyaraka ya makala Wikipedia:Makala kwa ufutaji tangu Agosti 2017 hadi Disemba 2018.

Kwa nyaraka za zamani zaidi angalia hapa.

Haieleweki, ni zaidi mahubiri mafupi kuliko makala. Kipala (majadiliano) 12:58, 7 Septemba 2017 (UTC)[jibu]

Imefutwa.--Baba Tabita (majadiliano) 18:57, 15 Septemba 2017 (UTC)[jibu]


Nimeweka alama ya "FUTA" juu ya makala hii; naona ni makala ya kwanza ya mchangiaji mpya sitaki kumkatisha tamaa lakini hii haiwezi kubaki jinsi ilivyo. Florah ana nafasi ya kuisahihisha karibuni. Nataka kumsifu kwa sababu alijaribu tayari kufanya utafiti na kutafuta vyanzo.

  • A) Abadilishe lugha na kuandika kama makala ya kamusi. Hadi sasa alianza kama mchango wa majadiliano si makala ya maelezo. Atazame katika ukurasa wa Wikipedia:Mwongozo_(Anzisha_makala) na kurasa nyingine za mwongozo.
  • B) Achungulie makala zilizopo! Aliweka kiungo kwa makala ya Kiingereza Dead Sea, basi pale anaweza kuona upande wa kushoto chini kiungo kwa makala ya Kiswahili juu ya mada hiyohiyo. Iko tayari makala ya "Bahari ya Chumvi" ambalo ni jina lake la Kiswahili jinsi ilivyotumiwa tangu miaka mingi katika lugha za Biblia inapotaja ziwa hili. Kama "Bahari Mfu" imekuwa jina linaloeleweka, basi unaweza kuiongeza katika sentensi ya kwanza ya makala ya Bahari ya Chumvi.
  • C) Unaweza ama kuongeza habari za madini katika makala iliyopo AU kama unataka ktunga makala mpya unahitaji kutafuta habari za undani zaidi. Madini au Chumvi gani? Asilimia? Chanzo? Je ziko tayari tasnia zinazovuna / chimba madini haya? Yapi? Ni madini gani yanayoaminiwa kuchangia kwenye tiba?
  • D) Kama unahitaji ushauri ulizia tu! Utapata. Kipala (majadiliano) 23:18, 8 Januari 2018 (UTC)[jibu]

Fupi sana, inakosa habari za kimsingi, haielezi kazi yake, haina data juu ya maisha yake, hakuna vyanzo. Ifutwe Kipala (majadiliano) 18:25, 6 Februari 2018 (UTC)[jibu]

Imefutwa. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:04, 22 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Makala inajaa madai mengi yasiyo na ushuhuda. Makala kuhusu mtu aliye hai zinatakiwa kuwa na ushuhuda. Makala inanipa picha ya kufanana na matanganzo ya kibiashara kwa kitabu hiki. Hakuna ushuhuda ya kwamba madai kuhusu umuhimu na ubora wa kitabu ni kweli. Nimeona tayari ya kwamba Mwashinga aliandika makala juu yake yeye mwenyewe. Kuna pia majina mwengine ambayo yanaleta picha ya kwamba alianzisha akaunti kwa jina tofauti kwa kuendeleza kujiandikia makala. Sioni sababu ya kumpa nafasi zaidi hapa kwetu. Kipala (majadiliano) 00:26, 9 Februari 2018 (UTC)[jibu]

Sijaisoma bado hii. Nijaribu kuisoma labda? Walau tuamue pamoja. Kuna zingine nimefuta moja kwa moja nikiwa natumia AWB bila majadiliano. Munisamehe kwa kweli.--MwanaharakatiLonga 02:34, 9 Februari 2018 (UTC)[jibu]

Nimeona mapendekezo ya makala husika na ninaweza kuona hoja yake ya Mhe Kipala. Hata hivyo mapendekezo yangu siku zote yamekuwa kuboresha makala kuliko kufuta. Naona makala hii ni mpya na inanafasi ya kuboreshwa. Kama wahariri wakiihariri na kuongeza ushuhuda unaokidhi sioni sababu kwa nini ifutwe. Tunazo makala nyingine zenye mapungufu lakini hatujazifuta kwa sababu tunaamini kwamba tukitoa muda wa kutosha ama mwazishaji wa makala au mhariri mwingine anaweza kuziboresha. Nashauri makala kama hizi tuzipe muda wa kukua. Sisi wote tunajua kwamba makala zinazohusiana na historia ya kitabu fulani au hata shairi moja moja si kitu kigeni katika Wikipedia za lugha nyingine. Nadhani tuwatie moyo wahariri waanzishe makala nyingi za aina hizi. Tuwe wavumilivu. Londrosi

Makala hii imeandikwa vizuri sana, na hata ushuhuda upo katika tanbihi. Sioni sababu za kufuta makala hiyo! --Baba Tabita (majadiliano) 05:43, 10 Februari 2018 (UTC)[jibu]
Oliver, huyu katumia marejeo kutoka katika kitabu husika. Si kama katoa marejeo kutoka nje. Sawasawa na kutafsiri wimbo na kutoa maoni yaleyale kutoka katika wimbo na kutumia kama marejeo. Hivyo basi, soma upya na ufungue macho yako. Umelubuniwa!--MwanaharakatiLonga 07:08, 18 Februari 2018 (UTC)[jibu]
Nimejaribu kuweka mambo sawa. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:05, 22 Julai 2018 (UTC)[jibu]

(pendekezo la kufuta lilipelekwa na Riccardo) - ni Kiswahili cha kompyuta, haieleweki. Itafsiriwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 19:42, 17 Februari 2018 (UTC)[jibu]

Imerekebishwa. Ibaki. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:05, 22 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Jaribio la kutafsiri sehemu ndogo za makala ya Kiingereza, tafsiri haikufikia kiwango cha kuitwa "Kiswahili", bila vyanzo, bila jamii, maelezo hayatoshi, hakuna viungo vya kutosha. Ama mtu aihurumie na kuitafsiri upya au ifutwe. Kipala (majadiliano) 20:21, 25 Aprili 2018 (UTC)[jibu]

Nimerekebisha. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:03, 22 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Sioni maana yoyote na haieleweki.ifutwe.Kipala (majadiliano) 07:38, 27 Aprili 2018 (UTC)[jibu]

Imefutwa. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:05, 22 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Tafsiri ya kompyuta mbaya mno, haieleweki, iwende au kuandikwa upya. Kipala (majadiliano) 07:42, 27 Aprili 2018 (UTC)[jibu]

Nimerekebisha. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:06, 22 Julai 2018 (UTC)[jibu]
Asante. Ila naona udhaifu mmoja wa makala maana mtungaji alitafsiri makala ya "patriotism". Nisipokosei uzalendo inamaanisha pia "nationalism" na hapa maana inakuwa tofauti. Sijui namna gani kuieleza katika makala kwa Kiswahili. Kutafsiri Kiingereza inaweza kutosha hapa? Kipala (majadiliano) 10:10, 23 Julai 2018 (UTC)[jibu]
Maana ya kawaida ya neno hilo ni patriotism, si nationalism. Shalom! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:04, 23 Julai 2018 (UTC)[jibu]

SD (rapa), Pato Machete-IMEFUTWA, Fermín IV-IBAKI, Dharius - IBAKI japo ni sentensi tatu tu hariri

Makala hizi hazieleweki, Kiswahili ni kibaya kiasi cha kusema tafsiri kompyuta au labda mchangiaji analiyejifunza Kiswahili kidogo sana lakini anajaribu kuandika hata hivyo. Ziandikwe upya au kufutwa. Kipala (majadiliano) 06:00, 30 Aprili 2018 (UTC)[jibu]

Nimefuta zisioeleweka kabisa.--Muddyb Mwanaharakati Longa 07:15, 28 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

Kiswahili kibaya mno, mwandishi hakijui. Isahihishwe au kufutwa. Kipala (majadiliano) 21:17, 15 Mei 2018 (UTC)[jibu]

Naona mumeisahihisha!--Muddyb Mwanaharakati Longa 07:11, 28 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

Hakuna ushahidi wala marejeo kuhusu kuwepo kwa imani hii. Inaonekana ni mzaha tu, ifutwe. Kipala (majadiliano) 19:40, 9 Juni 2018 (UTC)[jibu]

Imefutwa. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:07, 22 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Makala hii imetungwa na mwenyewe ambayo haiwezekani hapa wikipedia. Azimio la kuipendekeza kwa ufutaji si rahisi. Sehemu za makala zingeweza kukubaliwa lakini nyingine ni kama tangazo. Mwandishi ni mgeni kabisa maana makala hii inaonyesha muundo safi. Kama mtumiaji:Kibaka anapenda kuchangia nje ya kujitangaza ana uwezo wa kuchangia makala za maana. Ila tu makala hii inagusa kanuni zetu za kimsingi. Kipala (majadiliano) 15:27, 5 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Kibaka Unadhani unaweza kutetea hoja? Kifupi hivi, kijana ni kweli ana ubora wa vyote alivyoandika. Je, ni dhani kwa mwanawikipedia mmoja maarufu aliyeamua kujiandika na kuitumikia Wikipedia? NAWAZA kwa maapana namana ya kujibu hoja hizi. Wapo wanawikipedia wanaochangia na kuwa na makala zao. Japo sheria zipo, na zikavunjwa huko mawikipedia makubwa. Tazama HAPA orodha ya wanawikipedia wenye makala. Ni kweli mwandishi, ni kweli mjasiriamali, ni kweli meneja wa Harmonize. Kuna shida? --Muddyb Mwanaharakati Longa 06:47, 6 Julai 2018 (UTC)[jibu]
Si kitu kama kuna wanawikipedia wenye makala zao. Labda siku moja pia makala yako? Ila tu hao ni watu wenye kiwango cha umaarufu ili wametambuliwa na wengine, walionekana katika vyanzo vya kukubalika na wengine waliamua kutunga makala. Kamwe hao wenyewe. Hatuna orodha ya watu waliojaribu kutunga makala zao, lakini kama ingekuwepo ingekuwa ndeeeefu sana. ila tu makala hizi zimefutwa zote (isipokuwa wajanja waliokuwa hodari kujificha). --Kipala (majadiliano) 11:00, 6 Julai 2018 (UTC)[jibu]

...

Hoja yangu kubwa pia Muddyb ameitaja ikiwemo kuwa zaidi ya mimi kuwa mwandishi lakini mtu wa jamii na ninafanya pia yale niliyoyaoanisha kwenye kurasa niliyoianzisha, hivyo basi hakuna tofauti na mwingine akaitengeneza kama ilivyo sababu mimi nina utaalamu wa uandishi nikaamua pia sio mbaya kuiweka kwa sababu kuna wana jamii wangependa kujua upande wangu mwingine ambao ni wa muziki, Uandishi wa vitabu, Usimamizi wa kazi za kimuziki na vile vile ujasiriamali maana ni kweli vyote hivyo Mungu kanijaalia na vipo hata kwenye mitandao sio tu navijua mwenyewe. kiasi ukitafuta kwenye google jina Joel Vicent Joseph utakuta google pai wananitambua kama Tanzanian Author...--Kibaka

Kwa yote uliyotaja kuna nafasi pana sana kwenye ukurasa wako wa binafsi. Ukurasa wako wa mtumiaji utaonekana kwa mamilioni wa wasomaji. Lakini utaratibu wa wikipedia ni imara: hairuhusiwi kujitangaza kwenye article mainspace. Ingekuwa busara ukianza kuhamisha maudhui pale kabla ukurasa haujafutwa. Kipala (majadiliano) 09:56, 23 Julai 2018 (UTC)[jibu]
Kumbe alikuwa na kurasa mbili. Nimeelekeza ukurasa huu kwenda mwingine wa mtu huyohuyo. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:04, 22 Mei 2019 (UTC)[jibu]

Makala hii imenakiliwa kutoka Jiografia_ya_Tanzania#Tabianchi. Haina habari ya maana zaidi ya yale yaliyonakiliwa. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 14:48, 20 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Makala ilitungwa kifupi, nami niliiongezea habari kwanza kutoka Jiografia_ya_Tanzania#Tabianchi, halafu kutoka sehemu nyingine. Sidhani ni mbaya. Hata kama inafanana na mama yake, inaweza kuwa kichocheo kwa kuiongezea habari nyingine nyingi. Ni mada muhimu kimaisha kwa Watanzania wengi. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 15:09, 22 Julai 2018 (UTC)[jibu]
Umeiboresha, Asante. Basi ibaki. Kipala (majadiliano) 09:53, 23 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Loki inabaki hariri

Hata kwa Kiingereza ukurasa huu haupo. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:37, 28 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Nimeisahihisha. Inaweza kubaki.Kipala (majadiliano) 04:34, 21 Agosti 2018 (UTC)[jibu]

Kurasa nyingine hariri

Zimependekezwa zifutwe lakini hazimo katika ukurasa huu. Tazama: [[Jamii:Makala kwa ufutaji]]. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:37, 28 Julai 2018 (UTC)[jibu]

Hakuna matini ya Kiswahili. Umbo halilingani na masharti yetu. Hakuna vyanzo. Itafsiriwe na kusahihishwa au kufutwa. Kipala (majadiliano) 04:36, 21 Agosti 2018 (UTC)[jibu]

  Imefanyika.--Muddyb Mwanaharakati Longa 07:09, 28 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

Haiwezi kubaki. Ni mchangiaji mpya ambaye hajaelewa bado kuwa matangazo haya yanaweza kuwekwa kwenye ukurasa wake wa mtumiaji. Nilimandiki kuhusu hii, tumpe wiki moja kuhamisha matini kabla ya kufuta makala. Kipala (majadiliano) 19:02, 23 Agosti 2018 (UTC)[jibu]

Inawezekana ya kwamba makala hii ni kweli kuhusu mwandishi anayestahili kutajwa katika wikipedia. Lakini hakuna ushuhuda wowote, mfano kutaja jina la kitabu pamoja kampuni ya mchapishaji na mwaka wa kutolewa n.k. Pia kuna matini isiyo na maana yoyote (mfano majina ya marafiki). Haionekani kutokana na makala kama huyu ni kweli mtu aliyepata kiwango fulani ya umaarufu (aliwahi kutajwa katika gazeti au jarida au kitabu fulani?). Pamona na hayo matumizi ya HERUFI KUBWA hayalingani na utaratibu wa wikipedia. Linganisha Wikipedia:Mwongozo (Kutaja vyanzo), Wikipedia:Umaarufu. Kama hakuna masahihisho tunapaswa kufuta mchango huu. Kipala (majadiliano) 13:22, 25 Agosti 2018 (UTC)[jibu]

Nimerekebisha makala. Ibaki. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 09:15, 19 Februari 2019 (UTC)[jibu]

Makala hii inamhusu mchezaji anayeweza kustahili makala kama ushuhuda unapatikana. Lakini mwandishi haulingani kabisa na kamusi elezo haiwezi kubaki. Pia umbo na staili havilingani. Kama haisahihishwa afadhali kufuta. Linganisha Wikipedia:Mwongozo (Kutaja vyanzo) Kipala (majadiliano) 14:02, 25 Agosti 2018 (UTC)[jibu]

Msuva INABAKI KAMA Simon Msuva hariri

Makala hii inamhusu mchezaji anayeweza kustahili makala kama ushuhuda unapatikana. Hakuna vyanzo vilivyotajwa. Umbo la mwandishi haulingani staili yetu. Sehemu za matini (kama kuhusu mdogo wake) hazina maana kwa habari zake. Kama haisahihishwa afadhali kufuta. Linganisha Wikipedia:Mwongozo (Kutaja vyanzo). Kipala (majadiliano) 14:36, 25 Agosti 2018 (UTC)[jibu]

Ina afadhali sana. Isitoshe, ni kweli kuna mengine ya kupuuza. Ngoja nirudi tena. Lakini ibaki. Msuva ni mchezaji maarufu sana katika ligi kuu Tanzania Bara.--Muddyb Mwanaharakati Longa 13:59, 27 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

Nina mashaka kama makala hii ni sahihi. Wikipedia nyingine (dewiki, frwiki) zintaja jina hili kuwa eneo kwenye kisiwa kikubwa cha Java. Makala ya idwiki id:Mandiraja,_Banjarnegara inatumia picha ileile kwa kuonysha wilaya kwenye kisiwa cha Java. Pia Kiswahili cha makala ni kibaya. Sijakuta ushuhuda wowote kuhusu kisiwa cha Mandiraja. Heri tufute? Kipala (majadiliano) 05:17, 26 Agosti 2018 (UTC)[jibu]

Nimeona. Tufanyaje? Tubadili tufuate muundo wa Wikipedia nyengine au tuifute kama Wikipedia ya Kiingereza walivyofanya? Kuna mkanganyiko mwingi sana.--Muddyb Mwanaharakati Longa 08:54, 17 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

Kumbe ni mchango usiofaa wa mtu binafsi uliobaki tangu 2010! Basi ifutwe. Kipala (majadiliano) 16:50, 10 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

Si mahali pa kuandika mambo binafsi. Ifutwe!--Muddyb Mwanaharakati Longa 08:47, 17 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

Inaandikwa kama tangazo la biashara, ifutwe. Kipala (majadiliano) 20:48, 13 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

Hili ni tangazo. Naona haina haja kuwepo hapa. Ifutwe!--Muddyb Mwanaharakati Longa 08:46, 17 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

hakuna maelezo ya lemma mle, hakuna vyanzo kuonyesha habari ni kweli, na Kiswahili chake kibaya. Ifutwe. Kipala (majadiliano) 20:52, 13 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

Hofu ya Jumapili (Sunday Scaries) ni jambo lililo na umaarufu. Mengi yameandikwa kuhusu hisia hii katika wavuti kama Forbes, NBC news, thisisinsider, businessinsider na Thrive Global yote ambayo ni majalada yenye umaarufu Hreflafa (majadiliano) 11:13, 14 Septemba 2018 (UTC)[jibu]
Makala haina ushuhuda ya kwamba wataalamu wa saikolojia wameshafanya utafiti na kuthibitisha ya kwamba hii ni hali maalumu ya hofu. Nimeona tu utafiti moja kuhusu upatikanaji kwa hofu kali kwa nyakati tofauti ambako Jumapili iko mbele lakini haisemi ni hofu ya aina ya pekee [1] ila tu kutokea kwa hofu hasa siku ile kwa sababu ambazo bado hazieleweki.
Hasa sioni ufafanuzi wa "sunday scaries". Makala haisemi ni hofu ya nini. Kutoka makala siwezi kuona kama hii ni zaidi ya fesheni kati wa wanahabari na wanablogu huko Marekani. Tena makala inarudia matangazo ya kibiashara kuhusu athira za pipi hizi za cannabidiol gummy bears ambayo inaonyesha ya kwamba mada haijafanyiwa utafiti halisi.
Jina la makala limetafsiriwa tu kutoka Kiingereza bila kutambua ya kwamba utafsiri unabadilisha maana: Kwa Kiswahili inataka kujadili hofu ya Jumatatu inayotokea Jumapili,sivyo?
Nikipita kurasa za tovuti mbalimbali naona ufafanuzi tofauti kabisa: huko Marekani wanamaanisha ama ama hofu ya kuanza tena kazi baada ya wikendi bila kazi [2], au hali ya kujisikia vibaya baada ya siku 2 za ulevi mkali mtu anayona akiamka tena Jumapili alasiri au jioni[3]. Makala yenyewe haielezi kitu bali kurudia vipande-vipande kutoka tovuti bila kuonyesha utafiti.
Ingekuwa tofauti kama tungeona ushahidi wa makala za kitaalamu (au angalau tovuti inayorejelea utafiti wa kitaalamu, si tu sentensi fupi za wanasaikolojia waliohojiwa kuhusu hofu hii) pamoja na ufafanuzi unaoeleweka. Hatuna. Au kama tungepata makala kuhusu mashambulio ya hofu pamoja na habari ya kwamba hizi zinaweza kuzidi kwenye wikendi, yote kwa ushuhuda mzuri. Lakini jinsi ilivyo haiwezi kubaki, hasa isibaki chini ya lemma hii. Kipala (majadiliano) 12:41, 14 Septemba 2018 (UTC)[jibu]
Futa! Tupunguze mjadala.. ni biashara kaja kutangaza!--Muddyb Mwanaharakati Longa 08:38, 18 Septemba 2018 (UTC)[jibu]
Ni kweli kwamba mhariri huyo mara nyingi anaingiza propaganda ya biashara. Siku nyingine nimerekebisha, ila si kila mara. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:42, 19 Septemba 2018 (UTC)[jibu]

Huyu anaendelea kujinadi, kinyume cha sera za Wikipedia. --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:38, 29 Desemba 2018 (UTC) Makala hii isifutwe iendelee kujaziwa maelezo kwani Jabir Johnson ni kweli ni raia wa Tanzania na mwandishi wa habarina mtangazaji nchini humo.[jibu]

Hakuna maudhui yenye maana. Kipala (majadiliano) 13:20, 27 Septemba 2018 (UTC)[jibu]