Wikipedia:Kutotisha bali kukaribisha wageni kwenye wikipedia
(Elekezwa kutoka Wikipedia:Please do not bite the newcomers)
Wageni kwenye wikipedia ni watu muhimu sana kwa ajili ya maendeleo ya mradi wetu.
- Hadi sasa tuko wachache mno, tunamfurahi kila mmoja anayejiunga nasi.
- Wageni wanafanya makosa kwa sababu mbalimbali. Ni muhimu kuwasaidia kwa uvumilivu na upole.
- Haifai kupinga makosa yote wanayofanya. Tunaweza kusahihisha na kueleza masahihisho kwa lugha nzuri kwenye ukurasa wa majadiliano na katika hitimisho. Ni muhimu zaidi kuwasalimu, kuwaambia ya kwamba tuliona nafasi ya kuboresha lugha na umbo wa yale waliyoandika.