Wikipedia:Wakabidhi/2023-01-04 Miniti za kikao

TAARIFA YA KIKAO CHA WAKABIDHI wa SWWIKI TAREHE 04.1.2023

Waliohudhuria N/A Jina Nafasi 1 Ingo Koll (Kipala) Mwenyekiti (Mkutubi)

2 Idd Ninga Katibu (Mkabidhi)

3 Mohamed Lupinga (MuddyB) Mjumbe (Mkutubi)

4 Ricardo Riccioni Mjumbe (Mkabidhi) (aliingia lakini kutokana na matatizo ya mtandao alitoweka tena)

5 Antony Mtavangu (jadnapac) Mjumbe (Mkabidhi)

6 Eben Mlay (CaliBen) Mjumbe (Mkabidhi)

7 Aneth David (Asterlegorch367) Mjumbe (Mkabidhi)

8 Otto Nyongole (Olimasy) Mjumbe (Mkabidhi)

9 Justine Msechu Mgeni aliyealikwa

10 Anuary Rajabu Mgeni aliyealikwa

11 Husein Mbaga Mgeni aliyealikwa

12 Frank Kisamo Mgeni aliyealikwa

Agenda

   I. Kufungua Kikao na kuthibitisha Ajenda
   II. Kupeana taarifa na kazi tulizofanya
   III. users group Universities Students
   IV. Mpango wa mwaka
   V. Kurudisha Wikipedia ya Awali
   VI. Mengineyo

1. Kufungua Kikao na Kuthibitisha Ajenda Kundi la Wakabidhi wa Wikipedia ya Kiswahili tulikutana mnamo tarehe 4 mwezi wa pili kwa lengo la kufanya kikao kwa njia ya mtandao na kujadili mambo mbalimbali kuhusu Wikipedia ya Kiswahili na namna ya kufanya maboresho pamoja na kuweka mikakati mingine. Idd Ninga na Ingo Koll walijitolea kuandaa miniti za kikao. Katika kikao hiki,walialikwa pia wachangiaji wengine ambao siyo wakabidhi lakini ni wachangiaji ambao wamekuwa wakifanya maboresho katika makala nyingi na kuchangia mara kwa mara. Baada ya kikao kufunguliwa, wajumbe wote walipata nafasi ya kupitisha ajenda za kikao kama zilivyoandika katika barua pepe, na wote kwa kauli moja walikubali ajenda hizo zitumike katika kikao cha leo

2 Kupeana taarifa na kazi tulizofanya Wakabidhi pamoja na wahariri waalikwa walipata nafasi ya kuelezea kazi walizofanya pamoja na yale walio yaona wakati wa kuhariri au kuboresha makala.

Otto Nyongole alikuwa wa kwanza na alielezea kuhusu safari yake ya Arusha ambapo alikutana na wahariri wengine na kushauriana nao namna gani ya kuhariri makala katika Wikipedia ya Kiswahili, pamoja na hayo aliwaelezea sababu za makala kufutwa pamoja na sababu ya makala kuwekewa vigezo mbalimbali ikiwemo kigezo cha ufutaji wa makala. Idd Ninga, alielezea changamoto ya makala nyingi kutokuwa na vyanzo na makala zikaachwa hivyo hivyo bila ya kuwekewa kigezo chochote na kusema hilo linaweza kutazamwa kwa namna nyingine tena.. Aneth kwa upande wake alielezea kuwa kuna baadhi ya makala nyingine hazina vyanzo na yeye kama mkabidhi huwa anaziwekea kigezo cha chanzo lakini wakati mwingine kunakuwepo na makala muhimu sana ambazo zinahitajika lakini nazo pia zinakuwa hazina vyanzo,

Kipala alielezea mchango wa wahariri. Bado sehemu kubwa ya kazi inatekelezwa na Riccardo peke yake. Kwa bahati nzuri wahaririri walioalikwa leo ,Justine Msechu,Anuary Rajabu,Husein Mbaga pamoja na Frank Kisamo wamekuwa wakijitahidi kufanya maboresho katika makala mbalimbali katika Wikipedia ya Kiswahili, pia kuchukua sehemu kubwa ya taarifa za ukaribisho wa wageni.

Pia akaelezea kuhusu kupungua kwa idadi ya makala mbovu hasa zile zenye tafsiri ya Google. Sababu moja ni kupungua kwa editathons zilizoleta idadi kubwa ya hariri bovu. Nyingine ilikuwa utekelezaji wa utaratibu wa kuzuia mara moja wahariri wanaoleta tafsiri ya gooogle na kuwaruhusu tu kurudi wakikubali kuund amakala kwenye nafasi zao za watumiaji wadi zikubaliwe na mkabidhi. Kufuatana na maazimio ya awali, makala zisizoeleweka zinaweza kufutwa mara moja. Alisisitiza tunahitaji kuongezza usimamizi wa ubora.

Justine Msechu alipata nafsi na kusema ,kumekuwepo na makala nyingi ambazo hazina mvuto na kusema kwa sasa zinawekwa nguvu ili kuendelea kuboresha makala za aina hiyo

Husein Mbaga, katika maelezo yake alisema kuwa, katika ukurasa wa Ukaribisho hakuna maelezo ta kutosha kwa mgeni ya namna gani anaweza kuanzisha makala hali inayopelekea kutokuwepo kwa makala nzuri. Anuary Rajabu,alisema, kumekuwepo na makala ambazo hazina vyanzo pamoja na hayo zipo makala ambazo zimeandikwa kwa lugha isiyoelewa vizuri.

Vile vile,Ndugu Kisamo alielezea kuhusu kuwepo kwa makala nyingi ambazo hazina vyanzo ,pamoja na hayo, alielezea mfumo wa DATABOX kutokufanya vyema katika Wikipedia ya Kiswahili. Kipala aliongezea pia, zipo makala ambazo hazijaweka katika InterWiki (kuunganisha na lugha nyingine), na wahariri wengine wamekuwa wakishindwa kuweka link katika makala.

Swali liliulizwa katika kikao hiki ya nini kifanyike katika makala ambazo hazina vyanzo. Mjumbe mmoja alishauri, kuwepo na Editathon kwa ajili ya kuboresha makala ambazo tayari zimeandikwa ili kuongeza maboresho zaidi. Pia suala la watu kujifunza namna ya kuweza kuanzishwa kwa tempale kwa ajili ya maboresho,hili pia ni pendekezo kwa ajili ya wakabidhi wote, na ikasemwa pia, kama mkabidhi ukiona kuna sehemu inachangamoto, unaweza kuwasiliana na mwingine mwenye ujuzi Zaidi kwa ajili ya kuongeza maarifa .

Ilipendekezwa pia kwa waliopo Kilimanjaro na Arusha kuweza kukutana kwa ajili ya kujifunza kama nafasi itapatikana. Katika kikao hiki kulitolewa pendekezo la kukusanywa kwa topics ambazo watu wameona zinafaa kufanyiwa maboresho na topics hizi zinaweza kuwasilishwa katika kundi la Telegram

3. Msimamo kuhusu kundi la Universities Students (ajenda hii ilipelekwa mbele) Kikao kilijadili kuhusu ombi lilifanywa na Ndugu Magotech kuhusu kuanzishwa kwa kundi la Universities Students na ambapo tayari "Wikimedia Community User Group Tanzania" (WCUGT) pamoja na "Jenga Wikipedia ya Kiswahili" (JWK) walishatumiwa taarifa ya kuulizwa uwepo wa kundi hili. Katika maelezo ,ilielezwa kuwa Mago alianza kufanya kazi na kundi la WCUGT na baadae aliomba kusaidiwa ili kuendesha mafunzo kwa wanafunzi wenzake wa chuo alichokuwa akisoma,alifanyiwa ila baadaye. Zaidi alianza kufanya kazi kimya kimya bila kuishirikisha Wikipedia ya Tanzania.

Ilielezwa kuwa, Wikimedia Foundation (WMF) waliitaarifu Kundi la WCUGT pamoja na kundi la JWK kuhusu uwepo wa kundi hilo linalolenga wanafunzi wa chuo kikuu.

Antony alielezea pia kuhusu Community ya Arusha na kusema kuwa alifanya mawasiliano na Eben pamoja na Magotech ili kuweza kufahamu kuhusu malengo yao kama yanatofauti na malengo ya WCUGT na wote walisema kuwa hakuna tofauti ya kimalengo. Pia, Veronika kutoka Wikimedia Foundation, alimwuliza pia umuhimu wa kuwepo kwa makundi haya ndani ya Tanzania, ikihofiwa isije kutokea makundi mengi kama ilivyo nchini Nigeria

Mmoja wa wajumbe alisema kuwa hakuna shida yeyote kama makundi hayo mengine yataanzishwa ndani ya Tanzania kieneo maana ni kawaida kila kundi kupanga kazi yake. Ila mpango wa kundi la Mago „kuunganisha wanafunzi wote wa vyuo“ ni vigumu maana makundi yaliyopo huwa na wanafunzi pia, halafu haitakuwa rahisi kuunganisha wanafunzi wa miji tofauti.

Mwisho iliamuliwa kuwa, hatutoi msimamo wa pamoja kama wakabidhi na watakaoeleza msimamo watakuwa makundi yaliyotambuliwa na WMF ambayo ni WCUGT na JWK .

4. Mpango wa Mwaka Kikao kilichopita kilipendekeza kuandaa mpango wa mwaka. Antony anaeleza kwamba anaandaa mpango wa aina hii kwa ajili ya kundi la WCUGT kwa sababu WMF inaomba kupata maombi ya ufadhili kwa muda wa mwaka mmoja.

Ingo aliomba mpango huu uwasilishwe kwanza hapa kwenye mkutano wa wakabidhi ili tusipate tena hali ya kuona kwa ghafla editathons bila kujua kabla na kushtukizwa na mahariri yenye matatizo jinsi ilivyokuwa zamani. Antoni alikubali.

Shughuli zinazoweza kuwa na maana katika mwaka huu ni pamoja na

  • kumaliza makala za wabunge, ambayo ni pia zoerui nzuri kwa wageni; maana orodha ya wabunge imeshaandaliwa iko kama makala
  • mara serikali itatoa taarifa kamili ya sensa pamoja na data za kata, tunapata changamoto kuangalia upya makala za kata za Tanzania ; kazi ambayo itaongeza thamani kubwa kwa wikipedia ya Kiswahili maana makala zinazohusu Afrika Mashariki zinafunguliwa kushinda mengine.
  • ilipendekezwa kurudia jaraibio la kupata ufadhili kwa mashindano ya picha za kata iliyopelekwa na JWK miaka iliyopita lakini kukataliwa na WMF wakati ule; yakikubaliwa kuundwe kamati maalumu ya kushughulikia mashindano hayo ambayo itakuwa inaangalia picha bora.

Pia ilishauriwa kuwepo na Internet support kwa wakabidhi na wahariri ambao wanafanya kazi muda mwingine ili kuweza kusaidia makala nyingi kupitiwa na kuboreshwa zaidi, na hili linaweza kufanyika hata nje ya mashindano.


5. Kurudisha muonekano wa Wikipedia ya Awali Baada ya Muonekano wa Wikipedia ya sasa kuwa na changamoto na wahariri wengi kuona mfumo huo hautafaa na umekuwa changamoto kwa wahariri wengi hasa wahariri wapya kwa sababu mabadiliko hayo yanabatilisha sehemu ya kurasa zetu za msaada zulizoandaliwa kwenye msingi wa muonekano wa awali. Kipala aliweza kuwasiliana na Wahusika waliofanya mabadiliko hayo na kuwaeleza kuhusu makubaliano ya wahariri wa Tanzania kutaka kurejeshewa katika muonekano wa zamani, lakini wahusika hao hawakujibu chochote. Hivyo ilipangwa kutumwa rasmi kwa ombi la kutaka kurejeshwa kwa muonekano huo wa zamani. Ikakubaliwa pia, muonekano mpya uje mara baada ya kuwa kurasa za msaada katika Wikipedia ya Kiswahili zimefanyiwa marekebisho, lakini pia, Kigezo cha Ukaribisho kionyeshe namna gani mgeni anaweza kuwenda katika muonekano wa zamani , hasa kwa wakati huu ambao tunasubiri muonekano wa zamani kurudi. Antony alieleza kuwa malengo ya muonekano huu mpya ni kwa ajili ya kufanya maboresho ili yaje kuweza kusaidia hata watumiaji wengine ambao wanatumia vifaa vingine kama simu na muonekano huu utakuja kutumika katika Wikipedia zote, nae Otto alisema alishafanya survey kuhusu muonekano huo na kusema bado muonekano wa zamani unahitajika.

6. Mengineyo Katika mengineyo ilisemwa kwamba, tunaweza kutumia Ukurasa wa Wakabidhi kwa ajili ya majadiliano mambo mbalimbali yanayohusu Wikipedia ya Kiswahili. Pia, ilikumbushwa kuhusu mikutano ya Kimataifa ya Wikimania, na tayari nchi tatu za Afrika zimeomba kuandaa mkutano huo, nchi hizoni Tanzania,Rwanda na Kenya na hadi sasa mazungumzo bado yanaendelea ya nani ataanda mkutano huo.

Kufunga Kikao Baada ya majadiliano marefu,kikao kilifungwa na mwenyekiti hadi wakati ujao.

Arusha na Moshi 10.02.2023

Idd Ninga Ingo Koll Waandishi