Wilaya ya Meatu

Wilaya ya Meatu ni wilaya mojawapo ya wilaya tano za Mkoa wa Simiyu, Tanzania yenye postikodi namba 39400 [1]. Katika sensa ya mwaka 2002, idadi ya wakazi wa wilaya hiyo ilihesabiwa kuwa 299,619 [2].

Mahali pa Meatu (kijani) katika mkoa wa Shinyanga.

Makao makuu ya wilaya yapo Mwanhunzi. Eneo lake ni kilomita za mraba 8,835.

MipakaEdit

Meatu imepakana na Wilaya ya Bariadi upande wa kaskazini, Wilaya za Karatu, Ngorongoro na Mbulu upande wa mashariki, Mkoa wa Singida na Maswa upande wa magharibi na Sinyanga upande wa kusini.

Maeneo ya kuhifadhiwaEdit

Karibu nusu ya wilaya ni maeneo yaliyohifadhiwa ambayo ni

Maeneo mengine ya 4,582 km2 ni ardhi ya kilimo na ufugaji.[3]


Hali ya hewaEdit

Eneo la Meatu ni nusu yabisi yaani haipokei mvua nyingi. Kiwango cha mvua kinapungua kutoka kaskazini kuelekea upande wa kusini ambako ni milimita 400 za pekee zinazonyesha kwa mwaka ilhali sehemu za kaskazini zapokea milimita 900.. [4] Kiwango cha mvua huweza kuwa tofauti kila mwaka ambyo ni tatizo kwa ajili ya wakulima.

UchumiEdit

Uchumi kwa jumla ni wa kilimo na ufugaji. Mazao ya chakula ni hasa mahindi na mtama lakini kilimo cha mahindi huwa na matatizo ya mara kwa mara kutokana na mabaduiliko ya kiwango cha mvua. Kwa hiyo kila baada ya miaka mitano kuna uhaba wa chakula. Wanawake hulima mahali pengi viazi vitamu karibu na mito ya muda mahali ambako ipo.

Udongo hasa upande wa kusini una kiwango kikubwa mno cha magadi na hivyo hufai kwa kilimo cha muhogo ambalo ni zao linalovumulia ukame.

Ufugaji ni muhimu katika wilaya na wastani ya ng'ombe ni 12-13 kila kaya lakini kwa tofauti kati ya ng'ombe 0 na 2,00 kwa kaya.

Zao la biahara muhimu zaidi ni pamba. Watu wameanza kujenga vinu vya kuchambulia pamba kwa hiyo soko la pamba limeboreshwa hata kama mwendo huu unaweza kuleta matatizo ya chakula. Meatu ni eneo lenye pamba nyingi katika mikoa ya Simiyu na Shinyanga.

Utalii ni tawi la uchumi lililoanza kuchipuka kutokana na nafasi ya kuwinda.

Uchimbaji wa vito umeanza hapa na pale kwa kutumia mbinu za kienyeji.


MarejeoEdit

  1. https://www.tcra.go.tz/images/documents/postcode/tzPostcodeList.pdf
  2. Sensa ya 2012, Simiyu Region - Meatu District Council
  3. Site Report for Nzanza Village Meatu District, uk.5
  4. Site Report for Nzanza Village Meatu District, uk.5

Viungo vya NjeEdit

  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Simiyu bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.
  Kata za Wilaya ya Meatu - Mkoa wa Simiyu - Tanzania  

Bukundi | Imalaseko | Isengwa | Itinje | Kabondo | Kimali | Kisesa | Lingeka | Lubiga | Mbugayabanhya | Mbushi | Mwabuma | Mwabusalu | Mwabuzo | Mwakisandu | Mwamalole | Mwamanimba | Mwamanongu | Mwamishali | Mwandoya | Mwangundo | Mwanhuzi | Mwanjolo | Mwanyahina | Mwasengela | Ng'hoboko | Nkoma | Sakasaka | Tindabuligi