Tunduma ni mji wa Tanzania kwenye mpaka wake na Zambia. Kuna vituo vya mpakani kwa ajili ya usafiri kwenye barabara kuu ya TANZAM na reli ya TAZARA. Mji unaendelea upande wa Zambia kwa jina hilohilo. Msimbo wa posta ni 53901.

Mji wa Tunduma
Nchi Tanzania
Mkoa Mbeya
Wilaya Tunduma
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 219,309

Upande wa Tanzania Tunduma imekuwa halmashauri ya pekee katika mkoa wa Songwe; hadi mwaka 2012 ilikuwa kata ya Wilaya ya Mbozi[1].

Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, mji ulikuwa na wakazi wapatao 97,562 waishio humo, [2], waliongezeka hadi watu 142,943 mnamo 2016[3] na 219,309 katika sensa ya mwaka 2022 [4].

Pamoja na kuwa kituo cha mpakani ni pia njiapanda muhimu kwa sababu njia za kwenda Sumbawanga na wilaya ya Ileje zinaachana huko na barabara kuu ya TANZAM.

Marejeo hariri

  1. Tovuti rasmi ya Halmashauri ya Mji Tunduma
  2. "2012 Population and Housing Census General Report" (kwa Kiingereza). Government of Tanzania. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-05-11. Iliwekwa mnamo 2013-11-21. 
  3. [https://www.nbs.go.tz/nbs/takwimu/majimbo/MAJIMBOApril_Kisw.pdf Makadirio ya Idadi ya Watu katika Majimbo ya Uchaguzi kwa Mwaka 2016,Tanzania Bara]
  4. https://www.nbs.go.tz
  Kata za Wilaya ya Tunduma - Mkoa wa Songwe - Tanzania  

Chapwa | Chipaka | Chiwezi | Kaloleni | Katete | Majengo | Makambini | Maporomoko | Mpande | Mpemba | Muungano | Mwakakati | Sogea | Tunduma | Uwanjani


  Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Tunduma kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.