Wiliamu Tempier (Poitiers, Akwitania, leo nchini Ufaransa, karne ya 12 - Poitiers, 29 Machi 1197) alikuwa askofu mwenye busara na msimamo wa mji huo (kwa Kilatini Pictavium) kuanzia mwaka 1184.

Alitetea Kanisa lake dhidi ya maonevu yaliyofanywa na makabaila na alirekebisha maadili ya watu, akitoa mwenyewe mfano wa maisha yasiyo na dosari[1].

Tangu zamani anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe aliyofariki dunia [2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.