Willem van Genk
Willem van Genk (2 Aprili 1927 – 12 Mei 2005) alikuwa mchoraji na msanii wa picha kutoka Uholanzi, anayesifika kama mmoja wa wasanii maarufu katika Sanaa ya "Outsider". Maisha yake yote aliishi na changamoto kubwa za afya ya akili, akipitia dalili zinazohusishwa na tawahudi na skizofrenia. Kwa sababu ya mapenzi yake kwa treni, mabasi, na vituo vya treni, alijiita "Mfalme wa Vituo."
Mandhari ya miji na michoro zake zilizokatika-katika zinaonesha hisia zake kuhusu mamlaka za kisasa, hisia ambazo ziliathiriwa na baba mwenye tabia za unyanyasaji ambaye, kando na kumpiga, alimwachia kumbukumbu ya tukio la kusikitisha alilokumbana nalo kutoka kwa Gestapo wakati wa uvamizi wa Ujerumani nchini Uholanzi katika Vita vya Pili vya Dunia..[1]
Marejeo
hariri- ↑ Notably, this moniker is the title of the first monograph published on the artist, by his most trusted associate, Dick Walda. (For the evidence that Walda was van Genk's most trusted associate, see Nico Van Der Endt, Willem van Genk: Chronicle of a Collaboration, Amsterdam: Uitgave, 2014, p. 110. This book is available only in Dutch.)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Willem van Genk kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |