William England alifanikiwa kuwa mpiga picha wa victorian aliyependelea kuchukuwa picha stereoscopic.

William England in 1886

Vyanzo hawakubaliani tarehe yake ya kuzaliwa, lakini imenukuliwa na waandishi mbalimbali kwamba ilikuwa kati ya mwaka 1816 na 1830. Miaka ya 1840 Uingereza ilikuwa na studio ya daguerreotype potrait mjini London [1] Mwaka 1854 alijiunga na London Stereoscopic Company (LSC), ambapo mpiga picha Stereoscopic maarufu mwingine Thomas Richard Williams pia alikuwa hai wakati huo. baada ya muda England ikawa LSC's mpiga picha mkuu. Mwaka 1859 alisafiri kwenda Marekani kwa LSC na kuleta mfululizo wa stereoviews za USA na Kanada ambazo ziliwapa watazamaji wa Ulaya baadhi ya maoni Stereoscopic ya kwanza ya Amerika ya Kaskazini [2] Mwaka 1862 LSC ililipa guineas 3000 ili wapewe haki ya kipekee ya kupiga picha Maonyesho ya Kimataifa yaliyo kuwa yakifanyika Kensington Kusini, London. William England aliongoza timu ya LSC stereographers, ambayo ni pamoja na William Russell Sedgfield na Stephen Thompson, kuzalisha mfululizo wa stereoviews 350 za maonyesho [3]. Mwaka 1863 England alipiga picha Maonyesho ya Kimataifa ya Dublin, lakini baadaye mwaka huo aliacha kazi LSC na aka anza kujitegemea. Hatimaye alisafiri kote Ujerumani, Uswisi na Italia, akizalisha vitazamwe mfululizo zilizokusanywa kwenya mfululizo wa Alpine views 'iliyochapishwa chini ya mwamvuli wa Alpine Club' [4]

Katika miaka ya baadaye alikuwa hai katika mashirika kadhaa ikiwemo London Photographic Society na Photographic Society of Great Britain. Mwaka wa 1886 alikuwa mwanachama mwanzilishi wa Photographic Convention of the united Kingdom [5] Yeye aliaga duni mjini London mwaka 1896.

The nave from the Western Dome. Mtazamo Stereoscopic wa Maonyesho ya Kimataifa ya 1862 na William England iliyochapishwa na Kampuni ya London Stereoscopic

Vidokezo

hariri
  1. Lenman, Robin Ed (2005) The Oxford Companion to the Photograph, Oxford University Press
  2. Hannavy, John (2007). Encyclopedia of Nineteenth-Century Photography Routledge
  3. Tongue, Michael (2006) Expo 1862, Discovery Books
  4. Wettmann, Hartmut, William England’s 1869 Rhine Journey, Stereo World, Vol. 29 No. 1 available at: http://www.fotoplatz.stereographie.de/stwrld-WmE/ Archived 4 Machi 2016 at the Wayback Machine.
  5. British Journal of Photography, 10 Septemba 1886