William I wa Uingereza
Mfalme William I wa Uingereza (anayejulikana pia kwa jina la William the Conqueror, yaani William Mshindi, au kwa jina la Kifaransa kama Guillaume) alikuwa mtemi wa Normandy na mtawala wa mwisho wa nje aliyefaulu kuvamia Uingereza.[1]
William I "Mshindi" | |
---|---|
Mfalme wa Uingereza, Mtemi wa Normandi | |
William Mshindi jinsi alivyochorwa kwenye kitambaa cha Bayeux baada ya mwaka 1070 | |
Kusimikwa | 25 Desemba 1066 |
Amezaliwa | 1027 |
Mahala pa kuzaliwa | Normandi |
Amefariki | 9 Septemba 1087 |
Mahala alipofia | Rouen, Normandi |
Kuzikwa | Rouen |
Mwenza | Matilda wa Flanders (1031 – 1083) |
Mtoto | Robert II-mtemi wa Normandi, Richard-mtemi wa Benay, Adeliza, Cecilia, William II-mfalme wa Uingereza, Adela-mtemi wa Blois, Gundred, Agatha, Constance na Henry I-Mfalme wa Uingereza Robert II-mtemi wa Normandi, Richard-mtemi wa Benay, Adeliza, Cecilia, William II-mfalme wa Uingereza, Adela-mtemi wa Blois, Gundred, Agatha, Constance na Henry I-Mfalme wa Uingereza |
Jumba la Kifalme | Nasaba ya Normandi |
Baba | Robert 1, Mtemi wa Normandi |
Mama | Herleva |
Alizaliwa katika Normandy ambayo ni sehemu ya Ufaransa iliyokaliwa wakati ule na Wanormani waliokuwa watu wenye asili ya Skandinavia. Wazazi wake walikuwa mtemi Robert wa Normandi na mke wake wa kando Herleva. Baba alimpa cheo cha mtemi mteule alipokuwa na miaka 6 wakati alipoenda kujiunga na vita ya misalaba. Alipokuwa mbukwa alihitaji kupigania vita kwa miaka mingi dhidi ya watemi wadogo waliotaka kukamata cheo chake. Tangu mwaka 1054 alikuwa mshindi na kutokana na kifo cha mfalme wa Ufaransa aliweza kutawala Normandi kama mfalme mdogo.
Uingereza ilikaliwa wakati ule na Waanglia-Saksoni; lugha ya wakazi wengi ilikuwa Kianglia-Saksoni. Magharibi na kaskazini ya kisiwa cha Britania ilikuwa bado na wakazi asilia Wakelti na Wadenmark waliowahi kuunda makazi kwenye pwani ya mashariki. William alikuwa ndugu na mfalme Edward wa Uingereza (1042-1066) kwa sababu mama yake Edward alikuwa shangazi wa baba yake William. Edward alimtembelea William katika Normandi akamuahidia atakuwa mrithi wake. Lakini baada ya kifo cha Edward wakuu wa Uingereza walimchagua mtemi Harold kuwa mfalme mpya.
Hivyo William aliandaa jeshi kubwa kwa kusudi la kujipatia kile alichoona kama haki yake. Harold alimsubiri lakini alilazimishwa kuhamia Uningereza wa kaskazini kwa sababu jeshi kutoka Denmark ilivamia kisiwa. Baada ya mapigano mbalimbali Harold alishinda Wadenmark alipopata habari za uvamizi wa William aliyefikisha jeshi lake kwa jahazi kwenye kusini. Tarehe 14 Oktoba jeshi lake lililochoka kutokana na mapigano na matembezi lilikuta Wanormandi atika mapigano ya Hastings. Harold aliuawa pamoja na wengi wa wakubwa wake.
William aliendelea kukamata au kuua wakubwa wa Waanglia-Saksoni. Akagawa nafasi za utemi za kieneo kwa ndugu zake kutoka Normandi. Hiyvo alianzisha kipindi cha historia ya Uingereza ambako makabaila wenye lugha ya Kifaransa walitawala watu raia wenye lugha ya Kianglia-Saksoni na Kikelti.
Baada ya kukamata utawala William aliamuru kuandikwa kwa orodha ya miji na viji vyote na ugawaji wa nchi chini ya watawala wapya. Orodha hii linajulikana kwa jina la Doomesday Book (kitabu cha siku ya kiyama) kwa sababu alitangaza ya kwamba ugawaji wa mali na hali uendelee hadi mwisho wa dunia.
William alielazimishwa kutetea himaya katika vita nyingi yake dhidi ya viongozi wazalendo Waingereza waliozidi kuasi dhidi yake, uvamizi kutoka Denmark, Waskoti kutoka kaskazini na pia dhidi ya mfalme wa Ufaransa aliyejaribu kuwa tena mkuu juu ya Normandi.
Aligonjeka na kufa mjini Rouen (Ufaransa) mwaka 1087 alipopigana na jeshi la mfalme wa Ufaransa. Mwanawe Robert alikuwa mtemi wa Normandi na mdogo wake William II mfalme wa Uingereza. William Mshindi alizikwa mjini Rouen.
Marejeo
hariri- ↑ Key Stage Three History: The Study Guide (toleo la First). Coordination Group Publications. 2002. uk. 1. ISBN 1841463302.