Woga ni tabia ya kupatwa na hofu kupita kiasi inayokuwa ndani ya binadamu juu ya kitu au vitu fulanifulani. Wakati hofu ni ono la kawaida kwa binadamu na kwa wanyama wengi, woga ni tatizo la kisaikiolojia.

Mtoto mwenye hofu
Mfano wa hofu kwa wanyama: Paka kwa kawaida hupanda migongo yao wakati wa msongo wa mawazo au wasiwasi

Kila mtu anaweza akawa na woga wake, huenda ukawa juu ya Mungu, malaika, shetani, roho, lakini pia juu ya mnyama, mahali, kifo, mauaji, giza n.k.

Kila mmoja anatakiwa kujitawala asije akashindwa na tabia hiyo hata kuacha majukumu yake.