Yohane wa Mungu

Yohane wa Mungu (8 Machi 14958 Machi 1550) alikuwa mtawa wa Ureno alitoa huduma zake nchini Hispania.

Yohane wa Mungu
Sanamu ya Mtakatifu Yohane wa Mungu katika Vilar de Frades, Barcelos, Ureno.

Ametambuliwa na Kanisa Katoliki kuwa mtakatifu.

Sikukuu yake ni tarehe 8 Machi[1].

MaishaEdit

Yohane wa Mungu alizaliwa nchini Ureno mwaka 1495.

Baada ya kuishi maisha ya hatari kama askari, na akitamani kutumia maisha yake yaliyokuwa yamebaki kwa kufanya matendo mema, alijitoa mhanga kabisa ili awauguze wagonjwa.

Alianzisha hospitali huko Granada nchini Hispania, na yeye pamoja na wafuasi wake wakaunda Shirika la Wauguzi la Mt. Yohane wa Mungu.

Alijulikana sana kwa upendo wake kwa wagonjwa na maskini.

Alifariki huko Granada siku ya kutimiza umri wa miaka 55, tarehe 8 Machi, mwaka 1550.

Tazama piaEdit

TanbihiEdit

Viungo vya njeEdit

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.