Yohane wa Ravenna (karne ya 6 - Ravenna, Emilia-Romagna, Italia, 19 Januari 595) alikuwa askofu wa mji huo wa Italia Kaskazini wakati wa vurugu zilizotokana na uvamizi wa Walombardi[1].

Wakati Italia nzima ilikuwa inaharibiwa na vita dhidi yao, alishughulikia kwa ufanisi mahitaji ya Kanisa alivyoshuhudia Papa Gregori I.

Alijitahidi kusaidia wananchi kama alivyofanya mjini Roma Papa huyo aliyemuandikia kitabu "Regula Pastoralis" (yaani “Kanuni ya Kichungaji”).

Tangu kale anaheshimiwa na Kanisa Katoliki na Kanisa la Kiorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 19 Januari[2].

Tazama pia hariri

Tanbihi hariri

  Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.